Balozi wa kampuni
ya Hennessy, Cyrile Auriol akizungumza na Waandishi wa Habari asubuhi ya leo katika
ukumbi wa Kivukoni, ndani ya hoteli ya Serena, Dar es Salaam. Balozi Auriol alitua
Dar es Salaam jana akitokea Paris, Ufaransa na atakuwa nchini kwa ziara ya siku
tatu kabla ya kuelekea Nairobi kwa muendelezo wa ziara yake nchi za Afrika
Mashariki. Akiwa Dar es Salaam Balozi Auriol atahudhuria matukio mbalimbali, maalum
ya chakula cha jioni na uonjaji wa kinywaji hicho ambazo, zimeandaliwa ili
kuwazawadia watumiaji wa kinywaji hicho nchini ambao sasa wanafurahia kampeni
ya kinywaji hicho iitwayo ‘ Flaunt Your Taste’.
|