Cannavaro |
Na Mahmoud Zubeiry
WACHEZAJI
wawili wa Yanga, beki Nadir Haroub Ally ‘Cannavaro’
na mshambuliaji Said Rashid Bahanuzi wanaondoka leo saa 10:00 jioni kwa ndege
ya Qatar Airways kwenda China, kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa.
Cannavaro,
Nahodha Msaidizi wa Yanga ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba watakuwa huko kwa wiki
mbili na baada ya majaribio kama wakifuzu, klabu inayowataka itafanya
mazungumzo na klabu yao.
“Sisi wote
tuna mikataba na klabu, hivyo tukifuzu jamaa itabidi watuhamishe Yanga,”alisema beki huyo kati aliyezaliwa Februari 10, mwaka
1982.
Cannavaro yupo
Yanga tangu mwaka 2006, aliposajiliwa kutoka Malindi ya Zanzibar wakati Bahanuzi
amesajiliwa msimu huu akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Mwaka 2009,
Cannavaro alichukuliwa kwa mkopo na klabu ya Vancouver Whitecaps ya Canada na
baada ya miezi sita alirejeshwa Yanga alikoendelea kucheza hadi leo anakwenda
kujaribu bahati yake China.
Bahanuzi ameingia
na zali la aina yake Yanga SC, kwani katika mashindano ya kwanza kuichezea
klabu hiyo alifanikiwa kuibuka mfungaji bora wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki
na kati, Kombe la Kagame.
Hadi sasa, Said
Bahanuzi maarufu kama Spider Man,
ameifungia Yanga mabao 12 katika mechi 14, yakiwemo matatau ya penalti tangu
ajiunge na timu hiyo Julai mwaka huu.
Kwa sasa China ni nchi ambayo mastaa wengi waliokuwa Ulaya wanakwenda
kumalizia soka yao, mfano washambuliaji wawili wa zamani wa Cheslea, Didier Drogba
na Nicolas Anelka waliopo Shenghua Shanghai. Anelka ni kocha mchezaji.
Said Bahanuzi |