Azam FC |
Na Prince Akbar
LIGI Kuu ya soka ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea
leo kwa mechi tatu za viporo kuchezwa kwenye viwanja vitatu tofauti.
Wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Simba, Mtibwa
Sugar leo wataikaribisha JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
Coastal Union nao watashuka kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga
kumenyana na Polisi Morogoro, huo ukiwa mchezo wa kwanza tangu wafungwe mabao
4-1 na Azam wiki iliyopita
Azam FC, wakiwa na kumbukumbu ya kutandikwa mabao 2-0 tena
wakichezewa soka ambayo hawajawahi kuiona kwa timu nyingine yoyote ya Tanzania,
wao watakuwa kwenye Uwanja wao wa Chamazi, kumenyana na JKT Oljoro
Ligi hiyo itaendelea tena Jumamosi, Mgambo JKT ikimenyena na Azam FC Uwanja wa Mkwakwani,
Tanga, African Lyon na Mtibwa Sugar Chamazi, Dar es Salaam, Simba SC na Toto
Africans Taifa, Dar es Salaam, Prisons na JKT Ruvu Sokoine, Mbeya, Kagera Sugar
na Polisi Morogoro, Kaitaba, Bukoba na JKT Oljoro na Ruvu Shooting Uwanja wa Sheikh
Amri Abeid, Arusha.
Mechi nyingine ya
kuhitimisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu itachezwa Jumapili, Yanga wakiwa
wageni wa Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanfa.