ARSENAL SASA YATAKA KUMSAJILI ADEL TAARABAT IKIMKOSA ZAHA

Arsenal inataka kumsajili kiungo wa QPR, Adel Taarabt, mwenye umri wa miaka 23, iwapo mpango wao wa kumsajili winga wa Crystal Palace, Wilfried Zaha, mwenye umri wa miaka 19 itafeli.
Adel Taarabt
Kiungo wa QPR, Adel Taarabt anatakiwa Arsenal
Liverpool imeamua kukubali yaishe katika mpango wao wa kumsajili Didier Drogba, mwenye umri wa miaka 34, baada ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea kuamua kuelekeza nguvu zake kwa waajiri wake, Shanghai Shenhua ya China..
Roberto Mancini atamuomba Mkurugenzi wa Michezo wa Manchester City, Txiki Begiristain kumsajili kiungo mwenye umri wa miaka 29 wa Roma, Daniele De Rossi ifikapo Januari.
Newcastle United inakimbizana na mabingwa wa Italia, Juventus kuwania saini ya kiungo mwenye umri wa miaka 23 wa Toulouse, Moussa Sissoko.
Mchezaji anayetakiwa muda mrefu na Manchester United, Filip Djuricic, mwenye umri wa miaka 20, anayechezea Heerenveen, anaweza kuhamia Liverpool.

MANCINI AMEKALIA KUTI KAVU

Roberto Mancini na kibarua kizito cha kuwahakikishia wamiliki wa Manchester City, kwamba klabu hiyo iko kwenye mikono salama chini yake.
Rod Stewart
Gwiji wa muziki wa Rock, Rod Stewart 
Kocha wa Southampton, Nigel Adkins ataendelea kubakia katika nafasi yake angalau hadi baada ya mechi na Swansea mwishoni mwa wiki.
Kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere, mwenye umri wa miaka 20, amesema The Gunners lazima impe mkataba mpya Theo Walcott mwenye umri wa miaka 23.
Kinda wa Celtic, Tony Watt, mwenye umri wa miaka 18, amesema kufunga bao la ushindi dhidi ya Barcelona katika Ligi ya Mabingwa Ulaya "ni jambo zuri zaidi maishani mwake".
STEWART AMWAGA MACHOZI
Gwiji wa muziki w Rock, Rod Stewart alibubujikwa na machozi mara alipoona Celtic inapata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya vigogo wa Hispania, Barcelona.
Mshambuliaji wa QPR na England, Bobby Zamora, mwenye umri wa miaka 31, amesema kwamba licha ya kucheza soka ya ushindani, yeye si shabiki sana wa kandanda.