MICHUANO ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati,
CECAFA Tusker Challenge inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo miwili ya Kundi
A, kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole mjini hapa.
Wenyeji na mabingwa watetezi, Uganda, The Cranes watashuka
dimbani saa 12:00 jioni kumenyana na Ethiopia, mchezo ambao utatanguliwa na
mechi kati ya Sudan Kusini na Kenya, Harambee Stars, utakaoanza saa 9:00
Alasiri.
Mechi zote mbili zinatarajiwa kuwa kali na za kusisimua,
kulingana na matokeo ya awali ya mechi za Kundi hilo.
Cranes
iliilaza 1-0 Kenya katika mchezo wa ufunguzi, bao pekee la mshambuliaji wa
Saigon Xuan Thanh ya Vietnam, Geoffrey Kizito dakika ya 74, akiunganisha krosi
ya Iguma Dennis.
Ethiopia
iliifunga Sudan Kusini 1-0 pia, bao pekee la Yonatal Kebede Teklemariam na kwa
matokeo hayo, Korongo wa Kampala wanafungana na Ethiopia kwa kila kitu kwenye
Kundi A, kwa pointi tatu na bao moja kila timu.
Kenya pamoja
na kufungwa walicheza vizuri dhidi ya Uganda na kutengeneza nafasi ambazo walishindwa
kuzitumia, wakati wapinzani wao walifanikiwa kutumia nafasi hiyo moja.
Sudan Kusini
walicheza kwa kujihami zaidi siku hiyo, wakimuacha Nahodha wao, Hamisi Leon
pekee mbele.
Wakati
mchezo kati ya Uganda na Ethiopia, nchi pekee ya ukanda wa Afrika Mashariki na
Kati iliyofuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Afrika Kusini
unatarajiwa kuwa wa pande zote mbili, Kenya wanapewa nafasi kubwa ya kushinda
dhidi ya mwanachama mpya wa CECAFA, Sudan Kusini.
Kikosi cha
Uganda leo hakitarajiwi kuwa na mabadiliko makubwa sana na bila shaka kocha
Msoctland Bobby Williamson akawarejesha wale wale walioshinda dhidi ya Kenya;
Hamza Muwonge, Iguma Dennis, Godfrey Walusimbi,Henry kalungi, Isaac isinde,
Hassan Wasswa, Geoffrey Kizito, Moses Oloya, Emmanuel Okwi, Hamisi Kiiza na
Brian Umony.
Kwa Kenya,
bila shaka kikosi kitakuwa; Duncan Ochieng, Anthony Kimani, Abdallah Juma,
Jockins Atudo, David Owino, David Ochieng, Lama Salim Mohamed, Bernard Wanyama,
Humphrey Mieno, Anthony ‘Muki’ Kimani/Enock Obiero na Clifton Miheso/Paul Were.
MSIMAMO
KUNDI A:
P W D L GF GA GD Pts
Ethiopia 1 1 0 0 1 0 1 3
Uganda 1 1 0 0 1 0 1 3
Sudan Kusini 1 0 0 1 0 1 -1 0
Kenya 1 0 0 1 0 1 -1 0
MSIMAMO
KUNDI B:
P W D L GF GA GD Pts
Burundi 1 1 0 0 5 1 4 3
Tanzania 1 1 0 0 2 0 2 3
Sudan 1 0 0 1 0 2 -2 0
Somalia 1 0 0 1 1 5 -4 0
MSIMAMO
KUNDI C:
P W D L GF GA GD Pts
Rwanda 1 1 0 0 2 0 2 3
Eritrea 1 0 1 0 0 0 0 1
Zanzibar 1 0 1 0 0 0 0 1
Malawi 1 0 0 1 0 2 -2 0
VIWANGO VYA
UBORA FIFA
NCHI NAFASI
Uganda 86
Malawi 101
Ethiopia 102
Sudan 102
Rwanda 122
Burundi 128
Kenya 130
Tanzania 134
Zanzibar 134
Somalia 193
Eritrea 192
Sudan Kusini 200
(Viwango hivi vimetoka mwezi huu)