Na Ally Mohamed, Zanzibar
WAWAKILISHI
wa Zanzibar katika michuano ya Afrika mwakani, Super Falcon waliofuzu kucheza Ligi
ya Mabingwa Afrika na Jamhuri waliofuzu kucheza Kombe la Shirikisho wamejitoa
kwenye michuano hiyo.
Habari
zilizopatikana na kuthibitishwa na Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Aman
Ibrahim Makungu, zimesema kwamba timu hizo zimeamua kujitoa katika michuano
hiyo kwa sababu hazina fedha, ambapo kila timu ilihitaji kiasi cha dola za
Kimarekani 30,000, zaidi ya Sh. Milioni 45 kwa ajili ya maandalizi ya ushiriki
wa michuano hiyo.
Kufuatia
hatua hiyo ZFA, iko katika mazungumzo na baadhi ya klabu za Ligi Kuu ili kuona
kama kuna uwezekano wa kupata timu zitakazochukua nafasi hizo.
Mwaka huu
Zanzibar iliwakilishwa na timu ya Mafunzo katika ligi ya Mabingwa Afrika, huku
Jamhuri wakipata nafasi ya kushirki katika kombe la Shirikisho.
Hata hivyo
timu zote zilishindwa kufanya vizuri baada ya kuondolewa katika hatua ya mwanzo
katika michuano hiyo.