Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh Kanali mstaafu Fabian Massawe akisalimiana na waamuzi .PICHA ZOTE NA BUKOBASPORTS.COM
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh Kanali mstaafu Fabian Massawe akisalimiana na wachezaji wa timu ya Kagera sugar
Timu zote mbili zikimsikiliza mkuu wa Mkoa wa Kagera
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh Kanali mstaafu Fabian Massawe akisalimiana na wachezaji wa timu zote mbili Yanga na Kagera Sugar.Timu zikisalimiana kabla ya mtanange jioni hii
Kikosi kamili cha Yanga kilichopewa kichapo na wakata miwa wa Kagera Sukari jioni ya leo.
Kocha wa Kagera Abdallah King Kibadeni (kulia) na wasaidizi wake
Kocha wa Kagera Abdallah King Kibadeni akiendelea kufuatilia mtanange kwa makini
Bench la Wachezaji wa Kagera Sukari.
Said Bahanuz aliumia na nafasi yake ikachukuliwa Jerson TegeteSaid Bahanuzi akiendelea kujipoza na maumivu ya nyama za pajani baada ya kupata matatizo
Meza kuu
Mkuu wa mkoa wa kagera (katikati) akiwa na Malik Suddy Tibabimale(katibu chama cha mpira BKM) wakifatilia kwa makini mpambano kati ya Kagera Sugar na Yanga.
Kagera Sugar wakifanya mabadiliko
Hadi Half time hakuna timu iliyokuwa imemchungulia mwenzake.
Wapenzi wa soka Jukwaa la Golani maarufu kama Jukwaa la Balimi.Bench la timu ya Yanga
Wapenzi wa soka Jukwaa la Golani maarufu kama Jukwaa la Balimi. wakiangaliwa kwa makini Askari wa Ulinzi uwanjani hapo
Mdau wa Bukobasports.com akichukua matukio tayari kuyarusha live kwenye libeneke la bukobasports.com
Mashabiki jukwaa kuu
Mashabiki jukwaa kuu namuona Mr. Mbelwa mpenzi wa soka akiwa ameshika maji jukwaani na huku akiendelea kucheki mtanange
Wadau mbalimbali wakifatilia soka na mimi nilikuwa moja wapo baada ya kuonekana hapa
Mashabiki
Mashabiki
Katika mechi zilizochezwa jana, Simba SC ilizidi kujiimarisha kileleni kufuatia ushindi wa mabao 4-1 ilioupata kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya JKT Oljoro ya Arusha, ambayo ilimaliza pungufu ya wachezaji wawili baada ya kipa wake Shaibu Issa na mshambuliaji Meshack Nyambele kutolewa kwa kadi nyekundu kipindi cha pili.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh Kanali mstaafu Fabian Massawe akisalimiana na wachezaji wa timu ya Kagera sugar
Timu zote mbili zikimsikiliza mkuu wa Mkoa wa Kagera
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh Kanali mstaafu Fabian Massawe akisalimiana na wachezaji wa timu zote mbili Yanga na Kagera Sugar.Timu zikisalimiana kabla ya mtanange jioni hii
Kikosi kamili cha Yanga kilichopewa kichapo na wakata miwa wa Kagera Sukari jioni ya leo.
Waamuzi wa mpira wa kagera sugar na Yanga (OMARY JUMA - MWANZA, DOMINIQ NYAMSANA - DODOMA-HASSAN ZANI - ARUSHA - CHARLES MBILINYI- MWANZA NA JONESIA LUKYAA-BUKOBA)
Kikosi cha timu ya Kagera Sukari kilicho ifunga timu ya Yanga 1-0 kwenye uwanja wa kaitaba mjini hapaKocha wa Kagera Abdallah King Kibadeni (kulia) na wasaidizi wake
Kocha wa Kagera Abdallah King Kibadeni akiendelea kufuatilia mtanange kwa makini
Bench la Wachezaji wa Kagera Sukari.
Said Bahanuz aliumia na nafasi yake ikachukuliwa Jerson TegeteSaid Bahanuzi akiendelea kujipoza na maumivu ya nyama za pajani baada ya kupata matatizo
Meza kuu
Mkuu wa mkoa wa kagera (katikati) akiwa na Malik Suddy Tibabimale(katibu chama cha mpira BKM) wakifatilia kwa makini mpambano kati ya Kagera Sugar na Yanga.
Kagera Sugar wakifanya mabadiliko
Hadi Half time hakuna timu iliyokuwa imemchungulia mwenzake.
Wapenzi wa soka Jukwaa la Golani maarufu kama Jukwaa la Balimi.Bench la timu ya Yanga
Wapenzi wa soka Jukwaa la Golani maarufu kama Jukwaa la Balimi. wakiangaliwa kwa makini Askari wa Ulinzi uwanjani hapo
Mdau wa Bukobasports.com akichukua matukio tayari kuyarusha live kwenye libeneke la bukobasports.com
Mashabiki jukwaa kuu
Mashabiki jukwaa kuu namuona Mr. Mbelwa mpenzi wa soka akiwa ameshika maji jukwaani na huku akiendelea kucheki mtanange
Wadau mbalimbali wakifatilia soka na mimi nilikuwa moja wapo baada ya kuonekana hapa
Mashabiki
Mashabiki
Na Prince Akbar, Bukoba
BAO pekee la
Themi Felix katika dakika ya 67, jioni ya leo limewapa Kagera Sugar ushindi wa
1-0 dhidi ya Yanga SC, kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba katika mchezo wa Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Felix aliyeingia
kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mnigeria, Enyinna Darlington kwa kumtungua
bao hilo, kipa Mghana wa Yanga, Yaw Berko, ameendeleza rekodi yake kuvifunga
vigogo, Simba na Yanga katika Uwanja huo.
Hiyo inakuwa
mechi ya pili Yanga kufungwa ndani ya mechi sita walizocheza hadi sasa na mbili
wametoka sare- maana yake inabaki na pointi zake nane na kuzidi kujipunguzia
matumaini ya ubingwa msimu huu, ikiwa sasa inazidiwa pointi nane na vinara wa ligi
hiyo Simba SC.
Aidha, hii
ni mechi ya pili Yanga inacheza chini ya kocha wake mpya, Mholanzi Ernie Blandts
aliyerithi mikoba ya Mbelgiji, Tom Saintfiet na katika mechi hizo mbili ameambulia
pointi moja kutokana na sare dhidi ya Simba Jumatano.
Kwa ujumla
Yanga haijashinda hata mechi moja ya ugenini kati ya tatu ilizocheza hadi sasa,
ilitoka 0-0 na Prisons, ikafungwa 3-0 na Mtibwa na leo imechapwa 1-0 na Kagera
Sugar, wakati Alhamisi itacheza na Toto African mjini Mwanza.
Katika mechi
hiyo, Yanga ilipata pigo dakika ya 23 baada ya mshambuliaji wake mahiri na tegemeo,
Said Bahanuzi ‘Spider Man’ kuchanika nyama za paja dakika ya 23, baada ya kugongana
na beki Benjamin Effe wa Kagera Sugar na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi
yake ikichukuliwa na Jerry Tegete.
Tangu ajiunge
na Yanga akitokea Mtibwa Sugar msimu huu, leo Bahanuzi amecheza mechi ya 13 kwa
dakika hizo 23 na ameifungia timu hiyo jumla ya mabao 12, matatu kati ya hayo
kwa penalti.
Katika mechi
hiyo iliyochezeshwa na refa Omar Juma kutoka Mwanza, aliyesaidiwa na Dominick Nyamsana
wa Dodoma na Hassan Zani wa Arusha, kikosi cha Yanga kilikuwa; Yaw Berko, Juma
Abdul, Stefano Mwasyika/nurdin, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Athumani
Iddi ‘Chuji’, Nizar Khalfan, Frank Domayo, Didier Kavumbangu, Said Bahanuzi/Jerry
Tegete na Haruna Niyonzima.
Kagera;
Andrew Ntala, Jumanne Nade, Salum Kanoni, Amandus Nesta, Benjamin Effe,
Malegsesi Mwangwa, Daudi Jumanne, George Kavilla, Enyinna Darlington/Themi
Felix, Shijja Mkinna na Wilfred Emmeh/Paul Ngway.Katika mechi zilizochezwa jana, Simba SC ilizidi kujiimarisha kileleni kufuatia ushindi wa mabao 4-1 ilioupata kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya JKT Oljoro ya Arusha, ambayo ilimaliza pungufu ya wachezaji wawili baada ya kipa wake Shaibu Issa na mshambuliaji Meshack Nyambele kutolewa kwa kadi nyekundu kipindi cha pili.
Katika mechi
hiyo iliyochezeshwa na refa Amon Paul wa Mara, aliyesaidiwa na Anold Bugabo wa
Singida na Charles Simon wa Dodoma, hadi mapumziko Simba walikuwa tayari mbele
kwa mabao 2-1, mabao yake yote yakitiwa kimiani na kiungo Amri Ramadhan Kiemba
katika dakika za 16 na 44, wakati la Oljoro lilifungwa na Paul Nonga dakika ya
29.
Kiemba
alifunga bao la kwanza akiunganisha krosi pasi ya Christopher Edward, wakati
bao la pili lilitokana na krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’, yote kutokana na
mashambulizi ya upande wa kulia.
Ilikuwa
rahisi kwa Kiemba kufunga mabao yote akiwa kwenye eneo la hatari, kutokana na
mabeki wa Oljoro kumuwekea ulinzi zaidi Felix Sunzu.
Nonga naye
alifunga bao lake baada ya kupewa pasi ndefu na kumpiga chenga kipa na Nahodha
wa Simba, Juma Kaseja upande wa kulia mwa Uwanja na kuutumbukiza mpira nyavuni
kiulaini.
Bao hilo
lilitokana na beki Paul Ngalema kupokonywa mpira wakati amepanda kusaidia
mashambulizi na Oljoro wakafanya shambulizi la haraka.
Kipindi cha
pili Simba walirudi vizuri zaidi uwanjani na kuuteka zaidi mchezo- jambo ambalo
liliwafanya Oljoro wawapunguze kasi kwa kuwachezea rafu. Hilo liliwagharimu
kupoteza wachezaji wao wawili kabla ya filimbi ya mwisho na kufungwa mabao
mawili zaidi.
Dakika ya 83
Mganda Emanuel Okwi aliifungia Simba bao la tatu na katika dakika ya tatu ya muda
wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za mchezo, Okwi akiwa anaelekea kufunga
tena, alikwatuliwa na kipa wa Oljoro Shaibu Issa na refa akaamuru penalti
sambamba na kumtoa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja mlinda mlango huyo.
Awali ya
hapo, Oljoro ilimpoteza mchezaji mwingine, Nyambele dakika ya 78, ambaye
alionyeshwa njano ya pili kwa rafu aliyomchezea Jonas Mkude. Nahodha Kaseja
alitaka kwenda kupiga, lakini akazuiwa na Felix Mumba Sunzu akaenda kufunga bao
la nne kwa mkwaju wa penalti.
Kwa ushindi
huo, Simba imefikisha pointi 16 baada ya kucheza mechi sita, hivyo kuendelea
kuongoza Ligi Kuu, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 13, ingawa imecheza mechi
tano.
Katika mechi
nyingine za jana, Mgambo imepata ushindi wake wa kwanza baada ya kuichapa
Polisi Morogoro 1-0, wakati Toto African imeichapa JKT Ruvu 2-1 na Prisons
imelazimishwa sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar.