Wachezaji wa timu ya Yanga wakifanya mazoezi leo jioni katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba
Kikosi cha timu ya Yanga kimefanya mazoezi yake ya mwisho jioni hii katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba tayari kwa mchezo wake dhidi timu ya Kagera Sugar kesho katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom nchini Tanzania.
Akiongea na mtandao wa klabu www.youngafricans.co.tz , Kocha mkuu wa Yanga amesema anashukuru kwa kupata nafasi nyingine ya kufanya mazoezi katika uwanja ambapo watautumia kwa mechi ya kesho.
Wachezaji wote wapo fit, jana na leo wamefanya mazoezi wote hivyo naamini yoyote nitakayempanga kucheza mchezo wa kesho atafanya vizuri alisema 'Brandts'.
Aidha kocha Brandts amesema anashangazwa na hali ya uwanja wa Kaitaba jinsi ulibyo, kwani hauna matunzo kabisa na sehemu ya kuchezea ina mashimo, hali itakayolekea wachezaji kucheza kwa uangalifu.
Mchezo wa kesho Yanga itaingia uwanjani kupigana kufa na kupona ili iweze kuibuka na ushindi ambao utaisogeza katika nafasi nzuri tatu za juu na baadae kushika usukani wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania.
Yanga ambayo iliwasili jana asubuhi kwa shirika la ndege la Precison, ilifanya mazoezi jana katika uwanja wa Kaitaba na muda mchache baadae iliipata taarifa kwamba mchezo huo uliokuwa ufanyike leo jumapili umesogezwa mbele mpaka siku ya jumatatu, kupisha shughuli za kuuhamisha mwili wa aliyekuwa Kadinali wa kanisa katoliko Laurian Rugambwa.
Kufuatia mabadiliko hayo, Yanga itacheza na Kagera Sugar kesho siku ya jumatatu katika uwanja wa kaitaba na mchezo wake dhidi ya timu ya Toto Africans uliokuwa ufanyike siku ya jumatano mjini Mwanza umesogezwa mbele mpaka siku ya alhamisi.