Na Prince Akbar
MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Yanga na
Ruvu Shooting iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na
kumalizika kwa wenyeji Yanga kushinda mabao 3-2, imeingiza Sh. 47,615,000.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface
Wambura ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, watazamaji 8,233 walikata tiketi
kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh.
15,000, na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 8,420,578.47 wakati
Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 7,263,305.08.
Amesema mgawo mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi
wa kituo sh. 120,000, kamishna wa mechi sh. 203,000, waamuzi sh. 381,000,
mwamuzi wa akiba sh. 70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina
(stadium technical support) sh. 2,000,000.
Amesema umeme sh. 300,000, maandalizi ya uwanja (pitch
preparation) sh. 400,000, ulinzi wa mechi sh. 3,500,000 wakati tiketi ni sh.
2,959,100. Gharama za mchezo sh. 2,806,859.49, uwanja sh. 2,806,859.49, Kamati
ya Ligi sh. 2,806,859.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
1,684,115.69 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh.
1,122,743.80.
Aidha, Wambura amesema Kamati ya Ligi ya TFF imeipa onyo kali
African Lyon kutokana na washabiki wake kuweka bango lililoandikwa ‘We believe
in 0777’ kwenye mechi yake dhidi ya Azam iliyochezwa Oktoba 6, mwaka huu Uwanja
wa Chamazi, Dar es Salaam.
Amesema bango hilo ambalo si la mdhamini wa Ligi Kuu ya
Vodacom halitakiwi kuonekana tena kwenye mechi ambazo African Lyon inacheza
vinginevyo Kamati ya Ligi itachukua hatua kali dhidi ya timu hiyo.
Amesema Kamati ya Ligi imezikumbusha timu zote zinazoshiriki
Ligi Kuu ya Vodacom kuzingatia kanuni zinazotawala ligi hiyo ili iweze
kuendeshwa kwa ufanisi.