Timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Yanga, imeifunga
Mgambo JKT ya vijana pia, bao 1-0 katika mchezo wa utangulizi, Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam, kabla ya kuanza kwa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara,
baina ya kaka zao, Yanga A dhidi ya Mgambo JKT ya Handeni, Tanga. Bao hilo
pekee lilitiwa kimiani na Clever Charles dakika ya 65.
|
Zuberi Amiri wa Yanga B, akichuana na Charles Domayo wa JKT Mgambo |
|
Joseph Banda wa Yanga B (25) akipasua ukuta wa Mgambo |
|
Meshack Ramadhani wa Yanga kushoto akigombea mpira na beki wa Mgambo |
|
Banda akifumua shuti mbele ya mabeki wa Mgambo, mmoja akijaribu kuzuia |
|
Notikel Masasi wa Yanga B akiwa chini ya ulinzi wa mabeki wa Mgambo |
|
Kocha Ernie Brandts akifuatilia vipaji Yanga B ikicheza na Mgambo |
|
Notikel Masasi wa Yanga B, akichuana na mchezaji wa Mgambo |
|
Clever Charles, mfungaji wa bao la Yanga B leo, akiwa benchi baada ya kupumzishwa. Kulia kwake ni Said Manduta. |