KIUNGO Jack Wilshere atarejea uwanjani rasmi kesho wakati Arsenal ikimenyana na Norwich katika Ligi Kuu ya England.
Kiungo huyo wa kimataifa wa England amekuwa nje kwa miezi 15 kwa sababu ya maumivu, lakini sasa anrudi tena kwenye kikosi cha kwanza.
Wilshere amecheza mechi tatu katika Uwanja ambao hauna mashabiki na sasa yuko fiti kwa kazi tena.
Yuko kwenye orodha ya kikosi kinachosafiri kwenda Carrow Road katika mfululizo wa Ligi Kuu.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger akiwa na Jack Wilshere mazoezini
Wenger anatumai kumuanzisha kiungo Wilshere kwenye kikosi cha Gunners katika Kombe la Capital One dhidi ya Reading, badaaye mwezi huu
Alex Oxlade-Chamberlain aikitaniana na Wilshere katika mazoezi viwanja vya London Colney