Ronaldo |
Katika mechi zake 100, Ronaldo amefunga mabao 37; bao lake la kwanza akifunga katika ushindi wa 2-1 timu yake ikifungwa na Ugiriki katika hatua ya makundi ya Euro 2004.
Akiwa ana umri wa miaka 27, Ronaldo anakuwa mchezaji wa tatu mwenye umri mdogo kufikisha idadi hiyo ya mechi, baada ya Wajerumani Lukas Podolski na Estonia's Kristen Viikmäe.
Nyota huyo wa Real Madrid amesema katika taarifa yake kwenye ukurasa wake wa Facebook, akizungumzia mechi zake 100.
"Nakumbuka ilikuwa Agosti 20, mwaka 2003 dhidi ya Kazakhstan kwa mara ya kwanza nilipovaa jezi ya Ureno ya timu ya taifa ya wakubwa,"alikumbushia.
Mabao 11 zaidi yatamfanya Ronaldo ampiku Pauleta kuwa mfungaji bora wa kihistoria wa Ureno na anahitaji mechi 28 zaidi kumpiku Luis Figo.
Kwa sasa, Ureno ina pointi tano katika Kundi F ikichuana na Urusi kileleni katika kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014.