Katibu wa TFF, Angetile |
Na Prince Akbar
BADO kizungumkuti kimeuzingira uchaguzi
Mkuu wa Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA). Hiyo inafuatia Kamati ya Uchaguzi
ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kusema imekamilisha usikilizaji rufaa
zilizokatwa dhidi ya Kamati ya Uchaguzi ya DRFA na sasa hatima ya uchgauzi huo
itajulikana Oktoba 16, mwaka huu.
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah
Malabeja ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, ili kujiridhisha kuhusu uamuzi wote
uliofanywa na Kamati ya Uchaguzi ya DRFA kuhusu waombaji uongozi wote wa DRFA
waliopitishwa na ambao hawakupitishwa na Kamati ya Uchaguzi ya DRFA, Kamati
itatangaza uamuzi wake kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi wa DRFA siku ya
Jumanne, Oktoba 16, 2012.
Amesema kutokana na hali hiyo,
Uchaguzi wa DRFA uliokuwa ufanyike Oktoba 14, 2012 umeahirishwa hadi hapo
uamuzi kuhusu uchaguzi huo utakapotangazwa Jumanne, Oktoba 16, 2012.