Football | CAF Champions League
| |
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeteua marefa wapya wa kuchezesha mechi ya marudiano ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya mabingwa watetezi Esperance ya Tunisia na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Hatua hiyo inafuatia malalamiko yaliyowasilishwa na Mazembe dhidi ya refa Bakary Gassama kutoka Gambia.
Badara Diatta wa Senegal ndiye ambaye sasa atachezesha mechi hiyo itakayopigwa Jumamosi wiki hii mjini Tunis.
Wenyeji wanapewa nafasi kubwa ya kusonga mbele, baada ya kulazimisha sare ya bila kufungana wiki iliyopita mjini Lubumbashi.
Magazeti nchini Tunisia yamepinga uteuzi wa refa mpya kwa sababu anatoka nchi moja na kocha wa Mazembe, Lamine N’Diaye, ambaye ni Msenegal pia.
Mazembe ina washambuliaji hatari wa Kitanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu ambao wote kwa sasa ni tegemeo la timu hiyo.