Tegete katika mechi na Ruvu Shooting |
Na Mahmoud Zubeiry
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Jerry Tegete amesema kwamba sasa ameamua
kufanya kazi ili kurejesha heshima yake ambayo ilianza kupotea miaka ya
karibuni.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo Tegete, alisema kwamba kufunga
katika mechi mbili mfululizo zilizoipita ni salamu tosha kwa waliokuwa
wanaamini yeye ‘amekwisha’.
“Mchezaji ni kama binadamu yeyote, nilipitia wakati mgumu Yanga
miaka hii miwili iliyopita, ila kwa sasa namshukuru Mungu na ninawaahidi mashabki wa
timu yangu, Yanga, wasubiri mavituz zaidi.
Tegete alifunga katika ushindi wa 3-1 mjini Mwanza dhidi ya Toto na akafunga tena katika wa mchezo dhidi ya Ruvu Shooting, Yanga il,siio dala
Yanga Jumamosi ilitoka nyuma kwa mabao 2-0 na kushinda 3-2
dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam,lambalo alicheaz uziri.
Ushindi huo, unaifanya Yanga itemize pointi 14, baada ya
kucheza mechi nane, hivyo kujiweka sawa katika nafasi ya tatu, ikizidwa pointi
tatu na Azam inayoshika nafasi ya pili na pointi nne na Simba inayoongoza ligi
hiyo.
Hadi mapumziko timu hizo zilikuwa zimekwishafungana mabao
2-2, Ruvu Shooting wakitangulia na baadaye Yanga kusawazisha.
Mabao ya Ruvu yalifungwa na mshambuliaji Seif Abdallah dakika
ya tatu na lingine dakika ya 10, yote kutokana na mipira kutoka upande wa kulia
mwa Uwanja, la kwanza mpira wa adhabu na la pili krosi.
Ruvu, inayofundishwa na kocha na mchezaji wa zamani wa Yanga,
walitumia mwanya wa beki wa kulia wa Yanga, Oscar Joshua kutopata msaada wa
viungo wa timu hiyo anapopanda kusaidia mashambulizi.
Baada ya bao la pili, kocha Mholanzi, Ernie Brandts alimuinua
Juma Seif ‘Kijiko’ akitaka kufanya mabadiliko ya safu ya kiungo iliyokuwa
inaundwa na Nurdin Bakari upande wa ulinzi na Rashid Gumbo upande wa
mashambulizi, lakini hakufanya hivyo hadi kipindi cha pili.
Lakini haikuchukua muda mrefu wakati Kijiko ‘anatroti’ safu
ya kiungo ya Yanga iliyokuwa inaboronga ikaanza kucheza vizuri na kusaidia timu
hiyo kurudisha mabao hayo.
Rashid Gumbo aliangushwa nje kidogo ya eneo la hatari na
Mbuyu Twite akaenda kupiga mpira wa adhabu uliotinga moja kwa moja nyavuni
dakika ya 20 na haraka haraka Jerry Tegete akauchukua mpira kwenye nyavu za
Ruvu na kwenda kuuweka katikati.
Hilo lilikuwa bao la pili Twite anaifungia Yanga kwenye ligi,
ndani ya mechi nane alizocheza.
Krosi nzuri ya beki wa kulia, Juma Abdul iliunganishwa vema
kimiani na Tegete dakika ya 36 na kuifanya Yanga iwe sawa na Ruvu. Kutoka hapo,
Yanga waliuteka zaidi mchezo na walikaribia kufunga bao la tatu dakika ya 40,
kama pasi nzuri ya Didier Kavumbangu ingeunganishwa vema kimiani na Gumbo.
Kipindi cha pili Yanga walirudi na kasi tena na kufanikiwa
kupata bao la ushindi dakika ya 65, ambalo lilifungwa na Kavumbangu, baada ya
kutokea kizazaa langoni mwa Ruvu.
Baada ya bao hilo, Ruvu walizinduka nao kuanza kujibu kwa
mashambulizi langoni mwa Yanga na walikaribia kufunga mara mbili, mara moja
kipa Yawe Berko akiokoa na mara moja shuti la Seif Abdallah kugonga mwamba wa
juu ya lango na kurudi uwanjani, kabla ya Oscar Joshua kuondosha kwenye eneo la
hatari.
Baada ya mchezo huo, kocha wa Ruvu, Charles Boniface Mkwasa
pamoja na kujutia nafasi walizopoteza, lakini aliwalalamikia marefa wa mechi
hiyo kwa kuwapendelea Yanga, wakati kocha wa wapinzani wake, Mholanzi Ernie
Brandts alisema hawakuanza vizuri, lakini walitulia na kucheza vizuri, hatimaye
wakashinda- hivyo kuwapongeza vijana wake kwa kazi nzuri.
Katika mchezo huo, kikosi cha Yanga kilikuwa; Yanga
SC; Yaw Berko, Juma Abdul/Juma Seif, Oscar Joshua, Nadir Haroub
‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Rashid Gumbo/Shamte Ally, Nurdin Bazkari, Haruna
Niyonzima, Jerry Tegete/Hamisi Kiiza, Didier Kavumbangu na David Luhende.
Ruvu Shooting; Benjamin Haule, Michael Aidan, Baraka Jaffari, George
Assey/Mangasini Mbonosi, Ibrahim Shaaban, Ernest Ernest, Raphael Kyala/Ayoub
Katala, Hassan Dilunga, Seif Abdallah, Abrahman Mussa na Said Dilunga/Kulwa
Mobi.