Akuffo amefunga leo |
Na Princess Asia, Chamazi
SIMBA SC imeifunga Azam FC mabao
3-2 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika leo asubuhi kwenye Uwanja wa Chamazi,
maarufu kama Azam Complex, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Mabao ya Simba leo yamefungwa
Ramadhani Singano ‘Messi’, Uhuru Suleiman ‘Robinho’ na Daniel Akuffo, wakati ya
Azam yalifungwa na Jamil Mchauru na Khamis Mcha.
Hii inakuwa mechi ya nne Azam
inafungwa na Simba msimu huu katika mechi tano walizokutana hadi sasa, baada ya
awali kufungwa kwa penalti kwenye fainali ya Kombe la Urafiki, kufuatia sare ya
2-2, kufungwa 2-1 kwenye Nusu Fainali ya BancABC Sup8R na 3-2 kwenye mechi ya
Ngao ya Jamii, wakati wao walishinda 3-1 dhidi ya Wekundu hao wa Msimbazi,
katika Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Azam na Simba zitakutana tena katika
mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, mzunguko wa kwanza, Oktoba 27,
mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.