Emmanuel Okwi wa Simba akipiga mzito katika mechi ya jana na Olljoro |
Na Prince Akbar
MECHI ya
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Simba na Oljoro JKT ya Arusha
lililochezwa jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa wenyeji
kuibuka na ushindi wa mabao 4-1, imeingiza Sh. 46,680,000.
Ofisa Habari
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo ameiambia BIN
ZUBEIRY leo kwamba, watazamaji 8,081 walikata tiketi kushuhudia mechi
hiyo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila
klabu ikipata mgawo wa sh. 8,172,396.61 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)
iliyolipwa ni sh. 7,120,677.97.
Amesema mgawo
mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi wa kituo sh. 120,000, kamishna wa
mechi sh. 193,000, waamuzi sh. 210,000, mwamuzi wa akiba (reserve referee) sh.
70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (stadium technical
support) sh. 2,000,000.
Amesema umeme
sh. 300,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, ulinzi wa
mechi sh. 3,500,000 wakati tiketi ni sh. 3,175,000. Gharama za mchezo sh.
2,724,132.20, uwanja sh. 2,724,132.20, Kamati ya Ligi sh. 2,724,132.20, Mfuko
wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,634,479.32 na Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,089,652.88.
Wakati huo huo:
TFF imetoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama Soka Arusha (KRFA) uliochaguliwa
katika uchaguzi uliofanyika jana (Oktoba 7 mwaka huu).
Wambura amesema
ushindi waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi
wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ARFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia
mchezo huo mkoani Kigoma.
Amesema TFF
inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya ARFA chini ya
uenyekiti wa Khalifa Mgonja ambaye amechaguliwa tena kuongoza chama hicho.
“Uongozi huo
mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za
mpira wa miguu mkoani Arusha kwa kuzingatia katiba ya ARFA pamoja na vyombo vya
mpira wa miguu vilivyo juu yake. Pia
tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya ARFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa
kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za
wanachama wa TFF,”alisema Wambura.
Aliwataja viongozi
waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni Khalifa Mgonja (Mwenyekiti), Seif Banka
(Makamu Mwenyekiti), Adam Brown (Katibu), Peter Temu (Mjumbe wa Mkutano Mkuu
TFF), Omari Walii (Mwakilishi wa Klabu TFF) na Mwalizo Nassoro (Mhazini), wakati
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliochaguliwa katika uchaguzi huo uliofanyika
Leganga, Usa River ni Hamisi Issa, Athuman Mhando na Eliwanga Mjema.
Alisema bafasi
ya Katibu Msaidizi iko wazi na itajazwa katika uchaguzi mdogo utakayofanyika
baadaye.