// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SHEREHE ZA MTAKATIFU TOM KUSAINI 'UGALI MPYA' ZILIZOFANA YEMEN JANA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SHEREHE ZA MTAKATIFU TOM KUSAINI 'UGALI MPYA' ZILIZOFANA YEMEN JANA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, October 10, 2012

    SHEREHE ZA MTAKATIFU TOM KUSAINI 'UGALI MPYA' ZILIZOFANA YEMEN JANA



    Mtakatifu Tom katikati akisaini mkataba wa kuinoa Yemen na mabosi wake wapya (Picha zote kwa hisani ya Mtakatifu Tom)

    Na Mahmoud Zubeiry
    KOCHA Mbelgiji Tom Saintfiet aliyefukuzwa Yanga baada ya siku 80 za kuwa kazini, jana amesaini rasmi mkataba kuifundisha timu ya taifa ya Yemen katika sherehe zilizoifanyika mjini Sana’a.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY kutoka Sana’a, Yemen jana, Mtakatifu Tom alisema amefurahia mkataba huo mzuri na namna alivyopokewa kwa furaha na upendo katika ofisi mpya.
    “Nimefurahi sana, kila kitu ni kizuri, mazingira ya kufanyia kazi na watu waelewa pia, sasa ni jukumu langu kuwafurahisha watu wa Yemen kwa kuwatengenezea timu nzuri itakayowapa furaha kwa matokeo mazuri,”alisema Mtakatifu Tom.  
    Tom alisema kwamba anatarajia kuiongoza timu hiyo ya Magharibi mwa bara Asia katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Magharibi mwa Asia (kama Kombe la Challenge la CECAFA) itakayofanyika nchini Kuwait Desemba mwaka huu.
    Alisema katika michuano hiyo, amepangwa kundi moja na Saudi Arabia, Iran na Bahrain na Januari mwakani, ataiongoza timu hiyo katika Kombe la Gulf huko Bahrain.
    “Kwa sasa nipo katika Jiji la Sana'a na kesho nitaanza kazi kwa kambi ya kujiandaa na mchezo wa kirafiki Beirut, Oktoba 16 dhidi ya Lebanon,”alisema Mtakatifu Tom.
    Saintfiet alifukuzwa Yanga baada ya kutofautiana misimamo na uongozi wa Yanga, akiwa amefanya kazi siku 80 na kuiachia timu taji la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
    Saintfiet amefungwa mechi mbili Yanga katika mechi 14 alizoiongoza timu hiyo tangu ajiunge nayo, Julai mwaka huu, akirithi mikoba ya Mserbia, Kostadin Bozidar Papic.
    Katika mechi hizo, zimo sita za Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, ambazo aliiwezesha Yanga kutwaa taji, ikipoteza mechi moja tu dhidi ya Atletico ya Burundi.





    REKODI YA SAINTFIET YANGA
    1.     Yanga Vs JKT Ruvu             (Kirafiki)              2-0
    2.     Yanga Vs Atletico (Burundi, Kagame)               0-2
    3.     Yanga Vs Waw Salam (Sudan, Kagame)           7-1
    4.     Yanga Vs APR (Rwanda, Kagame)                   2-0
    5.     Yanga Vs Mafunzo (Z’bar, Kagame)                 1-1 (5-3penalti)
    6.     Yanga Vs APR (Rwanda, Kagame)                   1-0
    7.     Yanga Vs Azam (Kagame)                                2-0
    8.     Yanga Vs African Lyon (Kirafiki)                      4-0
    9.     Yanga Vs Rayon (Kirafiki, Rwanda)                  2-0
    10.                        Yanga Vs Polisi (Kirafiiki, Rwanda)          2-1
    11.                        Yanga Vs Coastal Union    (Kirafiki)         2-1
    12.                        Yanga Vs Moro United      (Kirafiki)         4-0
    13.                        Yanga Vs Prisons    (Ligi Kuu)                 0-0
    14.                        Yanga Vs Mtibwa (Ligi Kuu)                    0-3






    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SHEREHE ZA MTAKATIFU TOM KUSAINI 'UGALI MPYA' ZILIZOFANA YEMEN JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top