SHABIKI Aaron Cawley - ambaye aliingia uwanjani na kumshambulia mlinda mlango Chris Kirkland, amehukumiwa kifungo jela miezi minne.
SOURCE: http://www.dailymail.co.uk
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 21, kutoka Cheltenham, alimvamia kipa huyo wa Sheffield Wednesday katika mechi ya timu yake ya nyumbani, Leeds Ijumaa usiku na kumshambulia kwa sababu alikuwa anajiangusha kupoteza muda, timu hizo zikiwa zimefungtana 1-1.
Mwendesha Mashitaka, Paul Macaulay alisema Cawley aliiambia Polisi alifanya hivyo kwa sababu alikuwa amelewa na hakumbuki kabisa tukio hilo, ambalo limeonwa na mamilio waliotazama Televisheni.
Shabiki huyo akimshughulikia kipa Chris Kirkland