REAL MADRID YAMTAKA KIPA WA MAN UNITED DE GEA AKARITHI MIKOBA YA CASILLAS

BEKI SPURS ATAKIWA SOUTHAMPTON

Beki wa kati wa Tottenham mwenye umri wa miaka 28, Michael Dawson anatakiwa na Southampton wanaotaka kuimarisha safu hyao ya ulinzi, ambayo imeruhusu mabao 24 katika mechi nane za Ligi Kuu ya England msimu huu.
Tottenham ipo karibu kumnasa kiungo Mbrazil, Willian baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 wa Shakhtar Donetsk kusema kwamba anataka kucheza katika timu ya rafiki yake, Andre Villas-Boas.
Paris Saint-Germain imekanusha taarifa za kumtaka kiungo wa QPR, Adel Taarabt, mwenye umri wa miaka 23. Akizungumza na gazeti la Algeria, Le Buteur, rais wa klabu hiyo, Nasser Al-Khelaifi alisema: "Licha ya tetesi kwenye vyombo vya habari, hatujafanya mpango wowote wa kumchukua mchezaji huyo. Hadi sasa, hayupo katika mipango yetu."
Liverpool imepanga kumtokea mshambuliaji wa Schalke, Klaas-Jan Huntelaar ifikapo Januari. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29, mustakabali wake wa kuendelea kucheza Ujerumani haueleweki, baada ya kuahirisha mazungumzo ya mkataba mpya hadi Desemba.
Klaas-Jan Huntelaar
Klaas-Jan Huntelaar 
Real Madrid inamtaka kipa wa Manchester United, David de Gea, mwenye umri wa miaka 21, kama mrithi wa kipa wao namba moja kwa sasa, Iker Casillas. Kumekuwa na ubashiri kwamba, kipa huyo wa timu ya taifa chini ya umri wa miaka 21 anakumbuka nyumbani.
Kocha wa Leicester, Nigel Pearson anataka kuimarisha kikosi chake katika jitihada za kurejea Ligi Kuu kwa kumsajili mshambuliaji wa Stoke, Kenwyne Jones, mwenye umri wa miaka 28 kwa mkopo.

MCKINLAY KUWA MSAIDIZI WA STEVE KEAN

Kocha wa Fulham, Billy McKinlay anatakiwa na Blackburn ili akawe Msaidizi wa Steve Kean Uwanja wa Ewood Park. Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 43, ambaye amepiga kazi miaka mitano na Rovers kama mchezaji, pia anataka kumchukua shujaa mwingine wa zamani wa Blackburn, Chris Sutton awe msaidizi wake.
Mchezaji wa zamani wa Tottenham, David Ginola amesema kwamba winga Gareth Bale atakuwa mmoja wa wachezaji wakubwa duniani na ameweka bayana kwamba, Spurs itapata wakati mgumu kumbakiza mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales mwenye umri wa miaka 23, White Hart Lane.