KIUNGO wa Manchester United, Shinji Kagawa anakabiliwa na maumivu ya goti, ambayo yatamuweka nje ya Uwanja kwa wiki tatu hadi nne.
Kocha wa United, Sir Alex Ferguson amethibitisha habari hizo katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo.
"Kagawa atakuwa nje kwa wiki tatu hadi nne kutokana na maumivu ya goti. Aliumia katika mechi na Braga Jumanne katika Ligi ya Mabingwa,"alisema Mscotland huyo.
Shinji Kagawa akisikilizia maumivu katika mechi na Braga
Sir Alex Ferguson amesononeshwa na kuumia kwa nyota wake huyo
Katika hatua nyingine, Ferguson amesema beki Chris Smalling amerejea mazoezini baada ya kupona.
"Hiyo ni zawadi kubwa kwetu, Phil Jones anaanza mazoezi pia," alisema kuhusu Jones, aliyeumia goti mwezi uliopita mazoezini.
Chris Smalling aliyeruka juu, amerudi kazini