NICKI MINAJ AMTOLEA NJE BALOTELLI
WILLIAN KWA VYOVYOTE ANATAKA KUTUA CHELSEA
Kiungo mshambuliaji wa Kibrazi, Willian mwenye umri wa miaka 25, anatarajia kuhamia Ligi Kuu ya England licha ya klabu yake, Shakhtar Donetsk kutaka dau la pauni Milioni 25 ili kumuuza. Pamoja na hayo, mchezaji huyo anaweza kukubali kukatwa ili ahamie Chelsea au Tottenham.
Tottenham wanaweza kumkosa mchezaji wanayemtaka kwa udi na uvumba, Joao Moutinho baada ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 wa Porto, kuonyesha nia ya kuhamia Paris Saint-Germain Januari.
PSV Eindhoven ya Uholanzi inataka kubaki na kinda wake mwenye kipaji Riechedly Bazoer, ambaye ametimiza miaka 16. Pamoja na hayo, kinda huyo tayari amezivutia klabu nyingi za Ligi Kuu ya England, zikiwemo Manchester City, Arsenal na Newcastle.
Kiungo wa PSV, Kevin Strootman, mwenye umri wa miaka 22, amesema hatahamia Manchester United Januari, lakini Sir Alex Ferguson anaweza kuwasiliana naye tena baadaye.
Liverpool inamfuatilia kiungo kinda wa Anderlecht, Dennis Praet. Nyota huyo Ubelgiji mwenye umri wa miaka 18 alifunga baoe lake la kwanza katika timu ya wakubwa dhidi ya Ekranas kwenye mechi ya kufuzu Ligi ya Mabingwa, na Wekundu hao wameandaa pauni Milioni 4.
Mshambuliaji wa Spurs, Emmanuel Adebayor hataruhusiwa kuondoka Januari, amesema Kocha Andre Villas-Boas, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kutoanzishwa katika mechi hata mechi moja msimu huu.
UBAGUZI HAUTAISHA ENGLAND
Mshambuliaji wa zamani wa Aston Villa na Norwich, Dion Dublin haamini kama ubaguzi utaondolewa kabisa katika soka.
Mshambuliaji wa Marekani, Landon Donovan, mwenye umri wa miaka 30, amesema anaweza kukataa kwenda kucheza kwa mkopo kwa mara ya tatu Everton ili akafanye ziara ya kutembelea nchi mbalimbali dunian.
Fifa imeziambia kampuni zinazoendesha mchakato wa teknolojia ya langoni, Hawk-Eye na GoalRef kuweka bima iwapo klabu au Ligi zitachukua hatua za kisheria dhidi ya mfumo huo kwamba haufanyi kazi kwa usahihi.
Steve Coppell, Kocha wa Crystal Palace katika awamu nne tofauti zilizopita, anapewa nafasi ya kurithi mikoba ya Dougie Freedman, ambaye ameondoka Selhurst Park mapema wiki hii.
Habari kamili: the Times (subscription required)
Rais wa Uefa, Michel Platini amewaonya Serbia wanaweza kuchukuliwa hatua kali kwa kashfa ya ubaguzi hivi karibuni dhidi ya wachezaji wa kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 21 cha England U-21.
Rapa wa kike, Mmarekani, Nicki Minaj alikataa kukutana na mshambuliaji wa Manchester City, Mario Balotellibaada ya onyesho lake la hivi karibuni Jijini Manchester.