Na Prince Akbar
MTANZANIA Millan Mbise ameombewa Hati ya Uhamisho wa
Kimataifa (ITC) Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), itakayomwezesha kucheza
mpira wa miguu nchini Marekani.
Boniface Wambura, Ofisa Habari wa TFF, amesema Shirikisho la Soka
Marekani (USSF) limemuombea hati hiyo Mbise kama mchezaji wa ridhaa ili ajiunge
na timu ya Virginia Youth Soccer.
Wambura amesema klabu ya zamani ya Mbise aliyezaliwa Agosti
18, 1994 imetajwa kuwa Super Sport FC, na mechi ya mwisho kwenye timu hiyo
alicheza Novemba 15 mwaka juzi.
Amesema TFF inafanya mawasiliano na pande husika kabla ya
kutoa hati hiyo kwa mchezaji huyo kama ilivyoombwa na shirikisho hilo la
Marekani.