MOURINHO AAGIZA PAUNI MILIONI 50 ZITOLEWE GARETH BALE ATUE REAL MADRID
Jose Mourinho anawataka mabosi wake wa Real Madrid kutoa pauni Milioni 50 kumnunua winga wa Tottenham, Gareth Bale, mwenye umri wa miaka 23.
Chelsea iko tayari kuipa ofa ya pauni Milioni 48, Atletico Madrid kwa ajili ya mshambuliaji Radamel Falcao ifikapo Januari. Manchester City pia inamtaka mpachika mabao huyo mwenye umri wa miaka 26 kutoka Colombian.
Sir Alex Ferguson anataka kumsajili Ashley Cole, mwenye umri wa miaka, ahamie Old Trafford kama mchezaji huru, mara beki huyo atakapomaliza mkataba wake Chelsea msimu ujao.
Porto imetaja dau jipya la kumuuza winga wake kutoka Colombia, James Rodriguez, mwenye umri wa miaka 21, ambalo ni pauni Milioni 38. Mchezaji huyo anatakiwa na Manchester United.
Kocha wa Fulham, Martin Jol amesema kwamba mustakabali wa Brede Hangeland katika klabu hiyo bado uko shakani, wakati mazungumzo ya mkataba mpya na beki huyo mwenye umri wa miaka 31 yakiendelea.
DI MATTEO AAMUA KUWAPUUZA
Roberto Di Matteo ameamua kuachana na kuwafikiria makocha wapinzani wake, kuelekea mechi baina ya timu yake, Chelsea dhidi ya Manchester United kesho.
Beki wa Tottenham, Kyle Walker, mwenye umri wa miaka 22, amesema aliamua kuacha kutumia Twitter baada ya kupondwa na kukandiwa na mashabiki kiasi cha kuanza kuathiri kiwango chake cha uchezaji.