MECHI namba 79 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya
Mtibwa Sugar na JKT Ruvu (pichani) iliyopangwa kuchezwa Novemba 3, mwaka huu kwenye Uwanja
wa Manungu mkoani Morogoro, imesogezwa mbele hadi Novemba 7, mwaka huu.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface
Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba mabadiliko
hayo yamefanyika kwa vile Novemba 4 mwaka huu, Mtibwa Sugar itacheza mechi
namba 30 dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro.
Wambura alisema kwamba, mechi hiyo awali ilikuwa ichezwe
Oktoba 3, mwaka huu lakini ikabadilishwa ili kutoa fursa kwa mechi za Super
Week zilizoonyeshwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha Super Sport cha
Afrika Kusini.
|