Inside the mind of Mancini
KOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini amesema wachezaji wake 'mafaza' lazima wawe tayari kufiti katika mfumo wowote anaowataka wacheze- na amesema ni timu dhaifu tu inyaoweza kufa baada ya kufungwa mechi moja.
Matumaini ya City katika Ligi ya Mabingwa Ulaya yamepungua baada ya kufungwa na Ajax mjini Amsterdam juzi, huku wachezaji wakishutumu mfumo wa uchezaji wa Mancini kuiponza timu.
Huku timu yake ikiwa imefungwa 2-1, Mancini alimtoa Joleon Lescott na kucheza na mabeki watatu na hiyo ikaiponza timu kufungwa bao la tatu.
Akizungumza baada ya mechi, Micah Richards alisema kwamba wachezaji wenzake hawakuupenda mfumo alioutumia Mancini.
Roberto Mancini akitoa maelekezo kwa wachezaji wake
Mancini akiwaelekeza wachezaji wake kwa umakini kuelekea mechi ya kesho na Swansea
City bado wana maumivu ya kipigo cha Ajax
"Kama wewe ni mchezaji mkubwa haijalishi unatumia mfumo gani," alisema Mancini. "Kama huulewei mfumo kama huo, huwezi kuchezea timu kubwa.
Alichosema Micah si muhimu. Alijibu swali. Naelewa watu wanataka kuandika juu ya hili, lakini kwangu haina tatizo.
Labda Micah hakujua, kwa sababu ni mechi yake ya kwanza baada ya miezi miwili na nusu,"alisema Mancini.
City lazima ishinde mechi zake zote tatu za mwisho ili kufufua matumaini ya kuingia kwenye hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa.
Mancini amethibitisha Pablo Zabaleta ataukosa mchezo wa kesho dhidi ya Swansea baada ya kuumia nyama akiichezea timu yake ya taifa.
David Silva, Javi Garcia, Maicon na Jack Rodwell wanaendelea kupumzika katika 'wadi' ya majeruhi wa City.
Kocha wa City, Roberto Mancini (katikati) akiwasili Carrington mapema leo asubuhi
City siku wanapigwa na Ajax mjini Amsterdam
Mpinga mfumo wa Mancini, Micah Richards akipambana katika mechi ya juzi