KLABU ya Manchester United itaendelea kuitangaza DHL katika jezi zao mazoezi, baada ya kukubaliana na kampuni hiyo mkataba mpya wa udhamini wa jezi zao za mazoezi.
Wakati United inatangaza kuingia mkataba wa awali na DHL mwaka 2010 wenye thamani ya pauni Milioni 40 kwa miaka minne, ilikuwa ni kwa ajili ya maeneo yasiyo ya mkusanyiko wa watu na mechi za kufuzu za Ligi ya Mabingwa.
Rio Ferdinand akiwa na jezi ya DHL mazoezini ambayo imelipa pauni Milioni 40 kudhamini
Tangu hapo, United imepiga hatua nyingine kubwa ya kupata mkataba wa pauni Milioni 559 ya udhamini wa jezi na kampuni ya General Motors, ambayo inavunja rekodi ya dunia kwa kuchukua nafasi ya AON mwaka 2014.
Familia ya Glazer inayoimiliki klabu hiyo, imepiga hatua zaidi kwa kuinunua DHL, kuhakikisha wananufaika zaidi kwa mapato.
"Tumekamilisha vizuri mazungumzo ya mkataba wa udhamini wa jezi za mazoezi na DHL, mara utakapomalizika tu Juni 30, mwaka 2013," klabu hiyo ilithibitisha.
Familia ya Glazer