MAN CITY WAJIOSA WAZIMA WAZIMA NA 'MIFWEZA' YAO KUWANIA SAINI YA MKALI WA MABAO RADAMEL FALCAO
Manchester City inataka kumsajili mshambuliaji Mcolombia wa Atletico Madrid, Radamel Falcao, mwenye umri wa miaka 26, ifikapo Januari, kwa mujibu wa Skauti Mkuu wa vipaji wa klabu hiyo bingwa England, Carlo Cancellieri.
Mshambuliaji asiye na furaha Emmanuel Adebayor, mwenye umri wa miaka 28, amekuwa na mazungumzo makali juu ya mustakabali wake na kocha wa Tottenham, Andre Villas-Boas.
Sunderland imekubali kuingia mkataba wa muda mfupi na mshambuliaji mwenye umri wa miaka 29 wa zamani wa Everton, James McFadden, ambaye yuko huru hadi mwakani.
TERRY KUENDELEA NA UNAHODHA CHELSEA LICHA YA KASHFA YA UBAGUZI
John Terry, mwenye umri wa miaka 31, ataendelea kuwa Nahodha wa Chelsea, licha ya kufungiwa mechi nne kwa kashfa ya ubaguzi dhidi ya beki wa Queens Park Rangers, Anton Ferdinand.
Kocha wa Tottenham, Andre Villas-Boas anaamini kwamba sakata la Terry lilianza tangu Machi mwaka huu na ndilo lilimponza yeye kufukuzwa kazi katika klabu hiyo.
Kocha wa Manchester City, Roberto Mancini amesema kwamba bado ina imani na kipa wake Joe Hart, mwenye umri wa miaka 25, hata baada ya kukandiwa na Nahodha wa zamani wa Manchester United na mchambuzi wa Televisheni, Roy Keane juu ya bao alilofungwa dhidi ya Poland Jumatano.
Kocha wa Barcelona, Tito Vilanova amepuuza madai kwamba klabu hiyo imetengeneza video ya kushindana na beki wa kati wa Real Madrid, Pepe juu ya rafu anazocheza uwanjani.
Nyota wa zamani wa Queens Park Rangers, Rodney Marsh amesema kwamba ingekuwa sawa kwa klabu kumfukuza kocha Mark Hughes kama harakati za klabu kujinusuru na hatari ya kushuka Daraja.
Na Mark Hughes amemtetea Nahodha wa QPR, Park Ji-Sung, amekuwa akikandaiwa kwa kucheza kwa kiwango cha chini mwanzoni mwa msimu.
Kocha wa zamani wa Blackburn, Paul Ince anatajwa katika orodha ya makocha wanaowaniwa na Burnley.
Brendan Rodgers ameonya kwamba hatakuwa na maajabu ya haraka ya kuleta mabadiliko ndani ya Liverpool, baada ya mwanzo mgumu.
Beki wa Swansea, Angel Rangel, mwenye umri wa miaka 29, amesema kwamba si kweli hakukuwa na umoja kati yake na wachezaji wenzake dhidi ya kocha Michael Laudrup.
Kiungo wa Norwich, Elliott Bennett, mwenye umri wa miaka 23, amesema kwamba usalama katika klabu hiyo utawaondoa kwenye hatari ya kumaliza katika nafasi mbaya kwenye Ligi Kuu ya England.
Beki wa Wigan, Antolin Alcaraz, mwenye umri wa miaka 30, anaweza kurejea baada ya maimivu ya nyonga ndani ya saa 24.