Mama Chiku Gallawa |
Na Mashaka Mhando, Tanga
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Mama Chiku Gallawa anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi kwenye ufunguzi wa michuano ya Kombe la Taifa ya mpira wa Kikapu, Taifa
Cup mwaka 2012 yanayotarajiwa kuanza kesho kwenye viwanja vya Mkwakwani na
Harbours Club vilivyo jijini Tanga.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Kikapu Tanga (TRBA), Hamisi
Jaffary alisema maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri na waamuzi
kumi na mbili ambao watachezesha mashindano hayo tayari wameshawasili jijini
hapa tokea mwishoni mwa wiki.
Jaffary alisema mashindano hayo yataanza Octoba 29 na kufikia
tamati Novemba 5 mwaka huu na kushirikisha
mikoa mbalimbali hapa nchini ambapo mpaka juzi mikoa kumi na sita
ilikwisha kuthibitisha kushiriki mashindano hayo.
Mwenyekiti huyo aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Dar
,Arusha,Moshi,Iringa, Mbeya,Mara, Lindi,Shinyanga,Tabora,Dodoma na Tanga ambao ndio wenyeji wa mashindano
hayo ambapo alisema timu nyengine huenda zitathibitisha katika shirikisho la
mipira wa kikapu Taifa ikiwemo Zanzibar ,Unguja na Pemba.
Alisema mkoa wa Kigoma
walijitoa dakika za mwishoni kushiriki mashindano hayo ambayo msimu huu idadi
ya washiriki imeongezeka kutokana na kuongezwa kwa idadi ya mikoa.
Mashindano hayo wa mara ya kwanza yalifanyika jijini Tanga
1989 na mara ya mwisho ili kuwa ni 2005 msimu huu shamra shamra zimeonekana
kuwa ni muda kubwa kutokana na kuwa maandalizi ya maandalizi yanayofanywa na
mikoa shiriki huku viwanja ambazo zitatumika mashindano zimefanyiwa ukarabati
wa hali ya juu.
Mkoa wa Tanga unatarajiwa kuwa na wageni watapao 450 ikiwemo
wachezaji na viongozi wa timu ambazo zitashiriki michuano hiyo na kutoa wito
kwa wakazi wa Tanga kujitokeza kwa wingi kushuhudia michuano hiyo.
Aliongeza kuwa timu
zilianza kuwasili jijini Tanga
tokea Jumamosi na Jumapili ambapo kesho ndio ufunguzi rasmi wa mashindano hayo.