Dar
es Salaam 25, Oktoba 2012….. Mdhamini Mkuu wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,
kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, imewekeza katika kuwawezesha
mashabiki wa soka kupata taarifa na matukio ya mechi zote za ligi hiyo kupitia
njia ya simu za kiganjani na intanet.
Kupitia mifumo
mbalimbali ya kiteknolojia wateja wa Vodacom wataweza kupata matokeo ya mechi
mbalimbali kupitia simu zao za kiganjani ukiwa na ujumbe mfupi wa maneno na
mitandao ya kijamii.
Akizungumzia hatua
hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, amesema, Mtandao wa
Vodacom una miundombinu ya kutosha na unaongoza katika masuala ya teknolojia.
Hivyo itatumika katika kuwawezesha mashabiki wa soka walioko ndani na nje ya
nchi kujua matukio mbalimbali ya ligi
kuu ya Vodacom.
“Licha ya ligi yetu
kuonekana katika kituo cha Televisheni cha Super Sport. Tumejipanga sasa
kuhakikisha inakuwa katika mitandao mbalimbali muda wote kwa kila mchezo na
kila tukio katika soka, Mashabiki watapata taarifa za ligi popote
watakapokuwa,” alisema Meza na Kuongeza kuwa, “Kupitia intanet matukio haya yatapatikana kupitia Facebook na
Twitter na mitandao mingine ya kijamii.”
“Ili kupata matokeo
na taarifa mbalimbali kupitia njia ya simu mteja wa Vodacom atatakiwa kupiga *149*01# kisha atachagua VODACOM FLAVA na akisha kujiunga na
huduma hiyo itakayo muwezesha kupata taarifa na matokeo ya mechi mbalimbali”
Aliongeza kuwa, “ Kwa
wateja wanaotumia facebook na twitter kwao ni rahisi zaidi kwani huduma hizo
zinatolewa bure na Vodacom, hivyo mashabiki wa soka watatembelea Ukurasa wetu
wa facebook na Twitter na kupata taarifa mbalimbali kuhusu ligi na wengine kujishindia
zawadi kwa kujibu maswali mbalimbali zikiwemo tiketi za mechi za ligi,”
Aidha Mkurugenzi huyo
alitoa Pongezi kwa Vyombo vya habari kwa kazi kubwa inayofanya katika
kuwahabarisha watanzania kuhusu michezo mbalimbali hususani ligi kuu ya Vodacom
kupitia Televisheni, Radio, Magazeti na Mitandao ya kijamii.
“Vyombo vya habari ni
wadau wakubwa na wanafanya kazi nzuri sana katika kutoa taarifa hizi
wanastahili pongezi, nasi tunaangalia namna ya kuwaunga mkono kwa namna moja
ama nyingine katika jitihada za kukuza soka la Tanzania na tunaamini tutafika
mbali.”
Mkurugenzi huyo
alihitimisha kwa kutoa pongezi kwa timu mbalimbali zinazoshiriki katika ligi
kwa kusema kuwa zimeonesha hamasa kubwa na kubainisha kuwa ni ishara ya ukuaji
wa soka katika soka la Tanzania ambalo ndio lengo kuu la Vodacom.
“Ligi sasa imekuwa na
msisimko kila timu inajitahidi kushinda kila mech,hadi sasa timu zote zimeonesha
kiwango kikubwa na soka la kuvutia tunatarajia maendeleo haya yataleta tija
hata kwa timu yetu ya Taifa kufanya vizuri. Vipaji vingi vinaonekana na ajira
kwa vijana imeongezeka kupitia michezo,”
alihitimisha Meza.
Kampuni ya Vodacom
katika kuongeza msisimko kwa mashabiki wa ligi imetoa ofa mbalimbali msimu huu
kwa kuwawezesha wateja wake kupata SMS 50, Muda wa maongezi wa dakika 30 na MB
50 kwa shilingi 400 Ili kuwasiliana na ndugu jamaa na marafiki. Pamoja na mambo
mengine kampuni hiyo inaangalia namna ya kutoa adha ya ukataji tiketi kwa wateja
wake kutumia huduma ya M - pesa kununua tiketi za mechi mbalimbali.
Amir Maftah wa Simba katika mechi dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga |