Wachezaji wa Moro United wakimdhibiti mchezaji wa Simba (kushoto) katika mchezo wao wa kujipima nguvu kabla ya kuanza Ligi daraja la Kwanza wiki iliyopita. Moro inaanza na Villa Squad Mlandizi |
Na Prince Akbar
LIG Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL) inatarajiwa kuanza
kutimua vumbi leo kwenye viwanja mbalimbali nchini.
Kundi A kutakuwa na mechi tatu ambapo Burkina Faso itacheza
na Mbeya City kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati JKT Mlale itakuwa
mwenyeji wa Small Kids kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea.
Nayo Kurugenzi itaumana na Majimaji katika Uwanja wa Wambi
ulioko Mufindi mkoani Iringa. Kundi hilo litamaliza raundi ya kwanza keshokutwa
(Oktoba 25 mwaka huu) kwa mchezo kati ya Mkamba Rangers na Polisi Iringa
utakaofanyika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Mechi za kundi B kwa leo ni Ndanda dhidi ya Transit Camp
katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara na Villa Squad itakipiga na
Moro United kwenye Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi. Oktoba 25 mwaka huu ni
Green Warriors v Tessema (Mabatini, Mlandizi) na Polisi Dar v Ashanti United
(Uwanja wa Chamazi).
Kundi C leo ni Kanembwa FC v Polisi Dodoma (Uwanja wa Lake
Tanganyika, Kigoma), Mwadui v Morani (Kambarage, Shinyanga), Pamba vs Polisi
Mara (Kirumba, Mwanza) na Rhino Rangers vs Polisi Tabora (Ali Hassan Mwinyi,
Tabora).