LAMPARD KUUNGANA NA BECKHAM LA GALAXY JANUARI
Los Angeles Galaxy itajaribu kumsajili kiungo mkongwe wa Chelsea, Frank Lampard, mwenye umri wa miaka 34, aungane na mchezaji mwenzake wa zamani wa kimataifa wa England, David Beckham, mwenye miaka 37, ifikapo Januari.
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers amepanga kumsajili winga mwenye umri wa miaka 23 wa Arsenal, Theo Walcott na mshambuliaji wa Chelsea, Daniel Sturridge, mwenye umri kama huo pia.
Kiungo mkabaji, Sergio Busquets, mwenye umri wa miaka 24, anatarajiwa kuondoka Barcelona msimu ujao na Chelsea ina matumaini ya kumnunua kwa pauni Milioni 25. Mapema wiki hii, mabingwa wa Ligi Kuu, Manchester City walikanusha taarifa kwamba wanammezea mate mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania.
Tottenham Hotspur inaweza kumnunua winga wa Crystal Palace, Wilfried Zaha ifikapo Januari. Kinda huyo mwenye umri wa miaka 19, pia amekuwa akifuatiliwa na Spurs na Arsenal.
CHELSEA SASA KUMTEMA JOHN TERRY
Chelsea haitampa mkataba mpya beki wake mwenye umri wa miaka 31, Nahodha wake, John Terry atakapomaliza mkataba wake wa sasa msimu ujao kwa sababu ya tuhuma zake zinazomkabili sasa za kutumia kauli za kibaguzi na pia kushuka kwa kiwango chake kwa muda mrefu sasa.
Pia kuna shaka ya kupokonywa Unahodha kwa John Terry, baada ya wadhamini kadhaa kulalamikia nidhamu yake.
Kocha wa Newcastle, Alan Pardew inataka kuoiga mfumo unaotumiwa na Arsenal na timu NFL, NHL na NBA nchini Marekani katika vyumba vyake.
Ian Holloway anatarajiwa kupewa ofa ya kuwa kocha wa Blackburn. Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 49 wa zamani wa Blackpool, anaweza kuahidiwa 'ugali' huo ifikapo Januari na wamiliki wa Rovers, Venky, ili aisaidie timu hiyo kurejea Ligi Kuu.