KIUNGO wa zamani wa Simba SC, Hillary Fordy Echesa kwa sasa
anachezea klabu ya Muar FC ya Ligi Kuu ya Malaysia, yenye maskani yake mjini
Muar, Johor, aliyojiunga nayo msimu huu akitokea Tusker FC ya Kenya.
Klabu hiyo inatumia Uwanja wa Sultan Ibrahim uliopo Muar,
Johor na Echesa ni tegemeo katika klabu hiyo. Hii inakuwa klabu ya 10 kwa Echesa
tangu aanze soka ya ushindani mwaka 2001, alipoibukia Nzoia Sugar ya kwao,
ambayo aliichezea hadi 2003 alipohamia Ulinzi Stars, ambayo aliichezea hadi 2005
alipohamia Mumias Sugar, zote za Kenya na mwaka 2006 akajiunga kwa muda na
Yanga ya Dar es Salaam, ambayo iliachana naye akaenda Rayon Sport ya Rwanda mwaka
2006, alikocheza hadi 2008 akaenda Polis Di-Raja (PDRM FA) ya Malaysia, alikocheza
msimu mmoja na kujiunga na Deltras aliyoichezea 2009 kabla ya kutua Simba SC
mwaka 2010, ambayo baada ya msimu mmoja ilimtema akaenda Tusker ya kwao, Kenya
aliyoichezea kwa msimu mmoja na sasa amerejea Malaysia.
|
Echesa alipokuwa Simba SC |
|
Echesa akilima nyumbani kwake Nairobi |
|
Echesa alipokuwa Simba |
|
Echesa katika mazoezi ya ufukweni |
|
Echesa katika mazoezi ya gym |
|
Echesa nyumbani |
|
Echesa Malasyia |