Kim Poulsen |
Na Ally Mohamed, Zanzibar
KOCHA Mkuu wa timu ya soka taifa ya Tanzania,
Taifa Stars, Mdenmark Kim Poulsen anatarijia kuwasili visiwani Zanzibar kwa
ziara maalum kwa ajili ya kuangalia mechi za Ligi Kuu ya Zanzibar inayoendelea,
ili kupata wachezaji ambao atawateua katika kikosi cha Taifa Stars.
Akizungumza kwa njia ya simu,
mjumbe wa Kamati tendaji wa Zfa Taifa, Masoud Atai, amesema kuwa wamepokea
taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) ya ujio wa kocha huyo.
"Tumepokea taaifa kutoka kwa
wenzetu TFF, na barua wametuletea kwamba kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya
Tanzania, Taifa Stars atakuja Zanzibar kwa lengo la kuangalia mechi za ligi kuu
ya Zanzibar na kutizama wachezaji ambao watamfaa katika timu yake ya Taifa
Stars". Alisema Atai.
Kwa mujibu wa taarifa ya mjumbe
huyo ni kuwa Kim Poulsen anatarajiwa kuwasili visiwani Zanzibar tarehe 18 ya
mwezi huu na anatarajiwa kwenda kisiwani Pemba tarehe 19 ya mwezi huu na kukaa
huko kwa muda wa siku 3 kwa ajili ya kuangalia mechi za ligi kuu zitakazochezwa
katika kiwanja cha Gombani.
Kim Poulsen atarejea kisiwani
Unguja siku ya tarehe 22 ya mwezi huu kwa ajili ya kuangalia mechi za ligi kuu
katika uwanja wa Amaan. na anatarajiwa kuondoka visiwani Zanzibar tarehe 26 ya
mwezi huu.