Bahanuzi 'Spider Man' |
Na Mahmoud Zubeiry
MSHAMBULIAJI
tegemeo wa Yanga, Said Bahanuzi ‘Spider Man’ amechanika nyama za paja katika mechi ya Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inayoendelea kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba
dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar na kushindwa kuendelea na mchezo huo, akimpisha
Jerry Tegete.
Mfungaji huyo
bora wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame alicanika nyama dakika
ya 23, baada ya kugongana na beki Benjamin Effe wa Kagera Sugar na kudondoka
chini akiugulia maumivu.
Bahanuzi aliyeifungia
Yanga bao la kusawazisha kwa penalti dhidi ya mahasimu wao Simba Jumatano
iliyopita, ameiambia BIN ZUBEIRY kwa simu mida hii kutoka
Bukoba kwamba; “Nimechanika nyama, sijui itakuwaje, nasubiri daktari
atakaponiangalia zaidi,”alisema kwa masikitiko Said.
Tangu ajiunge
na Yanga akitokea Mtibwa Sugar msimu huu, leo Bahanuzi amecheza mechi ya 13 kwa
dakika hizo 23 na ameifungia timu hiyo jumla ya mabao 12, matatu kati ya hayo
kwa penalti.