KIUNGO Joey Barton ameshindikana na hawezekani popote! Tayari ameingia kwenye kashfa nyingine ya mchezo usio wa kiungwana akiwa katika klabu yake mpya, Marseille.
Kiungo huyo alijiunga na timu hiyo ya Ufaransa Agosti baada ya kufungiwa mechi 12 akiwa anachezea Queens Park Rangers msimu uliopita.
Lakini inaonekana Barton ameshindwa kubadilika kitabia hata baada ya kuhamia timu ya Ligue 1, baada ya kumchapa kiatu mchezaji wa Istre, Guy-Roland Niangbo.
Cheki Joey Barton anavyomtandika kiatu mchezaji wa FC Istres, Guy-Roland Niangbo katika mechi ya kirafiki
Hapa wanatenganishwa Barton na Niangbo baada ya kutaka kugombana
Hii inaweza kumuweka pabaya Barton anayejaribu kutafuta fitness ya kucheza mechi kabla ya kuanza kuichezea klabu hiyo kwenye ligi.
Lakini tukio hilo linakuja siku kadhaa baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 kukwaruzana na kipa wa AEL Limassol, Matias Degra katika Ligi ya Mabingwa.
Pia Barton haruhusiwi kucheza Ulaya, hadi Novemba 17 wakati Marseille itakapomenyana na Bordeaux.
Muingereza huyo alikiri hivi karibuni kwamba kadi nyekundu aliyopewa katika mechi ya mwisho ya Ligi Kuu England dhidi ya Manchester City, Mei mwaka huu ilimuangusha sana.
Barton anampa mtu kitu hapo..hebu cheki....
Barton aligombana na Carlos Tevez akapewa kadi nyekundu baada ya kugombana na wachezaji wengine wa City, Sergio Aguero na Vincent Kompany kabla ya kumvaa Mario Balotelli.
SOURCE: http://www.dailymail.co.uk