MWANASOKA wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi, Edgar Davids anaweza kucheza mechi yake ya kwanza usiku wa leo katika klabu ya Barnet baada ya kuajiriwa kama kocha mchezaji kwenye klabu hiyo ya Ligi Daraja la Pili ikimenyana na Northampton.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 39 na mshindi wa zamani wa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya amepewa jezi namba 38.
Edgar Davids anajiandaa kurudi uwanjani kuikoa Barnet isishuke Daraja la Pili
Davids amekuwa nje ya soka tangu astaafu mwaka 2010 akiwa na Crystal Palace, hadi alipoungana na Mark Robson katika klabu ya Barnet wiki iliyopita.
Kuwasili kwake kumeshindwa kufufua matumaini ya The Bees, pale walipofungwa 4-1 na Plymouth mwishoni mwa wiki iliyopita na timu hiyo kuendelea kuishi mkiani mwa ligi.
Davids akiishuhudia Barnet akiwa jukwaani ikimenyana na Plymouth
SOURCE: http://www.dailymail.co.uk