GWIJI wa soka Uholanzi, Edgar Davids alirejea uwanjani jana usiku akiiongoza kwa mara ya kwanza klabu ya Daraja la Pili, Barnet kupata ushindi wake wa kwanza msimu huu, baada ya kuilaza 4-0 dhidi ya Northampton.
Mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 39, ambaye amesajiliwa pia kucheza baada ya kuingia mkataba wa kuwa Kocha Msaidizi wa Mark Robson, ameonyesha bado wamo, kwani hakuwa anapoteza pasi na kukumbushia enzi zake alipoichezea mechi 74 Uholanzi na kung'ara na klabu za Ajax, Milan, Juventus na Spurs.
Kiwango chake jana kilitosha kabisa kumpa heshima ya mchezaji bora wa mechi hiyo.
Davids akimfunga mtu tela jana
Davids akishangilia na wenzake baada ya Andrew Yiadom kuwafungia bao
Barnet, ambayo imepata pointi tatu za kwanza ndani ya mechi 12, ilishinda mechi hiyo kutokana na mabao ya Krystian Pearce, Andrew Yiadom, John Oster na Anthony Edgar.
Akizungumza baada ya mechi hiyo, Davids alisema: "Najisikia kusema heshima ya Mchezaji Bora wa mechi ni kwetu sote, kwa sababu zilikuwa ni jitihada za timu.
Bado wamo, mcheki Davids anavyoteleza
SOURCE: http://www.dailymail.co.uk