MWANASOKA wa zamani wa kimataifa wa Senegal, El Hadji Diouf ameanzisha vita ya maneno na Steven Gerrard - akidai kwamba Nahodha huyo wa Liverpool ni mbinafsi.
Diouf amekuwa akikutwa na kasumba ya ukorofi katika klabu anayochezea na mshambuliaji huyo mtukutu sasa asahau kabisa kurejea Anfield.
Akiwa Leeds hivi sasa, mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 31 alichezea Wekundu hao kati ya mwaka 2002 na 2004.
El Hadji Diouf amemfungulia mdomo Steven Gerrard
"Gerrard alikuwa ananionea wivu wakati huo natikisa ulimwengu wa soka. Hakukuwa na mbinafsi zaidi yake... hajali kuhusu mtu yeyote.
"Gerrard yuko tayari Liverpool ifungwe, lakini yeye amefunga bao. Wakubwa wa Liverpool hawana cha kusema juu yake. Sikuweza hata kuanzishwa na [Jamie] Carragher."alisema.
Akiwa Liverpool, Diouf alifungiwa na kutozwa faini kwa kugombana na shabiki wa Celtic katika mechi ya Kombe la UEFA Uwanja wa Parkhead.
Nahodha wa Liverpool, Gerrard amepewa makavu na Diouf
Diouf sasa anajipanga upya kisoka akiwa Nahodha wa Leeds inayocheza Daraja la Kwanza, chini ya kocha Neil Warnock.
Klabu nyingine alizochezea ni Sochaux, Rennes, Lens za Ufaransa, Bolton, Sunderland, Blackburn za England, Rangers and Doncaster za Scotland lakini licha ya utukutu wake, hakuna shaka juu ya uwezo wake uwanjani.
"Siku moja nilikodi ndege na Maradona. Akanishika mkono na kusema anafurahia kuniona nacheza. Hiyo ilinifurahisha."alisema Diouf.
Ameichezea Senegal mechi 69 na amesema: "Rejea Senegal, mimi ni Mungu wao. Watu walifanya fujo kwa sababu sikuitwa kucheza mechi ya mchujo na Ivory Coast."alijigamba.
Diouf alikuwa mchezaji mwenzake Gerrard Liverpool kati ya 2002 na 2004
Read more: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2220097/Steven-Gerrard-selfish-Liverpool-says-El-Hadji-Diouf.html#ixzz29l8jWVpF
Follow us: @MailOnline on Twitter | DailyMail on Facebook