CHELSEA YATENGA PAUNI MILIONI 38 KUUNUNUA MTAMBO WA MABAO RADAMEL FALCAO

Chelsea imetenga dau la pauni Milioni 38 kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa bei mbaya, Mcolombia, Radamel Falcao mwenye umri wa miaka 26 ifikapo Januari, mwakani kutoka klabu ya Atletico Madrid, ambao nao pia wanajiandaa kumpa mkataba mpya mnono ili abaki.
Radamel Falcao
Falcao
Wakala wa Lewis Holtby mwenye umri wa miaka 22, shabiki wa Everton ambaye ameipagawisha Schalke na ambaye pia anatakiwa na Liverpool, amesema kuna ofa kutoka England na Hispania kwa ajili ya kiungo huyo.
Kocha wa Fulham, Martin Jol anajiandaa kupambana na klabu yake ya zamani, Hamburg kuwania saini ya mshambuliaji wa Catania mwenye umri wa miaka 24, Takayuki Morimoto, ambaye aliweka rekodi ya mchezajik mdogo zaidi kucheza Ligi Kuu ya Japana, akiwa ana umri wa miaka 15.
Manchester United na Arsenal zote zinamtaka kumsajili kinda wa Crewe, mwenye umri wa miaka 18, mshambuliaji Max Clayton.
REDKNAPP KUFUNDISHA DARAJA LA KWANZA
Kocha wa zamani wa Spurs, Harry Redknapp anajiandaa kwa mazungumzo ya kuwa kocha mpya wa Blackburn ya Daraja la Kwanza England.
Bosi wa Blackburn, Shebby Singh pia ameripotiwa kutaka kumpa ofa hiyo gwiji wa soka Argentina, Diego Maradona ili awe kocha mpya wa klabu hiyo.
Chama cha Soka England, kimepokea vielelezo vya mtafaruku uliotokea kwenye chumba cha marefa kubadilishia nguo Uwanja wa Stamford Bridge, uliowahusisha viongozi wenye hasira wa Chelsea, refa Mark Clattenburg na kiungo wa Blues, John Mikel Obi baada ya kufungwa na Manchester United JUmapili.
Nahodha wa zamani wa Arsenal, Tony Adams ameionya klabu hiyo kwamba haitamaliza ukame wa mataji wa miaka saba, iwapo itaendelea kuuza wachezaji wake nyota.
Kocha wa Fulham, Martin Jol amesema kuchagua wawili kati ya washambuliaji wake wanne - Dimitar Berbatov, Mladen Petric, Hugo Rodallega na Bryan Ruiz - ni matatizo ya raha.