Juan Mata amefunga mabao mawili ndani ya dakika mbili na kuzima matumaini ya Andre Villas-Boas kulipa kisasi cha kufukuzwa kazi Chelsea kwenye Uwanja wa White Hart Lane.
Villas-Boas, alifukuzwa Chelsea siku 226 zilizopita baada ya miezi minane ya kwua kazini na alifanikiwa kuongoza mechi ya leo kwa mabao ya William Gallas na Jermain Defoe, kabla ya The Blues kuzinduka dakika 20 za mwisho.
Juan Mata akishangilia mbele ya mashabiki wa Chelsea
TAKWIMU ZA MECHI
TOTTENHAM: Friedel, Walker, Gallas, Caulker, Vertonghen, Huddlestone (Livermore 67), Sandro, Lennon, Sigurdsson, Dempsey (Adebayor 74), Defoe. Subs not used: Lloris, Naughton, Dawson, Falque, Townsend.
NJANO: Walker, Gallas, Hudlestone.
WAFUNGAJI: Gallas dk46, Defoe dk54.
CHELSEA: Cech, Ivanovic, Luiz, Cahill, Cole, Ramires, Mikel, Oscar (Sturridge 83), Hazard (Lampard 90), Mata, Torres. Subs not used: Turnbull, Romeu, Moses, Azpilicueta, Bertrand.
NJANO: Ivanovic, Ramires.
WAFUNGAJI: Cahill dk18, Mata dk66, dk69, Sturridge dk90
REFA: Mike Dean (Wirral)
Mengi yamefanywa na Eden Hazard na Oscar tangu wawasili msimu huu, lakini alikuwa ni Mata, aliyesajiliwa na Villas-Boas msimu uliopita, ambaye aliutuliza mchezo huo kwa mashambulizi yake yenye akili.
Mspanyola huyo alifunga bao lake la tano msimu huu akitumia makosa ya Gallas na kisha akafunga bao lingine lililofanya wawe mbele kwa 3-2 akiunganisha pasi ya Hazard.
Roberto Di Matteo, aliyekuwa Msaidizi wa Villas-Boas msimu uliopita aliinuliwa kitini na Daniel Sturridge aloiyefunga bao liloifanya Cheslea ishinde 4-2.
Gary Cahill akiifungia bao la kwanza Chelsea
William Gallas alipoisawazishia Tottenham
Jermain Defoe akipasua ukuta wa Cheslea
Mata
Mata
Daniel Sturridge alitokea benchi kufunga la nne