Kell Brook ametimiza ndoto zake za kuwania ubingwa wa dunia, baada ya jana usiku kumtwanga Muargentina Hector Saldivia katika raundi ya tatu kwenye ukumbi wa Motorpoint Arena mjin Sheffield.
Bondia huyo Muingereza mwenye umri wa miaka 26, alionekana kumzidi mpinzani wake kuanzia kengele ya kwanza katika pambano lake la mwisho la mchujo kabla ya kuwania taji la IBF, uzito wa Welter ambalo anapenda kuligombea mapema mwakani.
Brook aliahidi kumtandika Saldivia ili kuilipia timu ya taifa ya soka ya England kisasi cha bao la Mkono wa Mungu la Maradona.
Kell Brook kulia akizipiga na Hector Saldivia
Brook akimpa kitu Saldivia
Brook amemkalisha chini Saldivia
Brook amemmaliza Saldivia kwa kumkalisha chini
Brook akishuhudia mpinzania wake akihesabiwa na refa Howard Foster
Brook akishangilia na mwalimu wake
Sasa ni mshindani Namba 1: Brook akishangilia na promota wake Eddie Hearn