KAMPUNI ya Coca Cola Kwanza, leo imewapa tuzo Waandishi watano wa Habari nchini, baada ya kuibuka vinara katika tuzo za Waandishi Bora wa mashindano ya soka ya vijana kwa umri chini ya miaka 17, Copa Coca Cola yaliyofanyika Julai mwaka huu.
Upande wa Blogs, bongostaz.blogspot.com ya BIN ZUBEIRY imeibuka kinara na kuzawadiwa Sh, Milioni 2 sawa na washindi wengine, upande wa Televisheni, Jimmy Tara wa ITV, Radio, Amry Masare wa Radio One, Magazeti, Japhet Kazenga wa Daily News na Mpiga Picha, Mohamed Mambo wa Habari Leo.
Tuzo hizo zilitolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma wa Coca Cola Kwanza, Evans Mlelwa, makao makuu wa kampuni hiyo ya vinywaji baridi, Mikocheni, Dar es Salaam.
Mchakato wa kutafuta washindi uliendeshwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), ambacho leo kiliwakilishwa na Katibu wake, Amir Mhando.
Baadhi ya Waandishi waliohudhuria wakiwa kazini |
BIN ZUBEIRY anapokea mzigo |
BIN ZUBEIRY anapokea mzigo |
Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi |
Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi |
Jimmy Tara anapokea mzigo wake |
Amry Masare anapokea mzigo wake |
Kazenga ana[pokea mzigo wake |