Balozi wa kampuni ya Glenmorangie, Bwana Niel Hendriksz,akizungumza na Waandishi wa Habari katika hoteli ya Hyatt Regency, Dar es Salaam, zamani Kilimanjaro. |
Balozi akikaribishwa kuzungumza na Meneja Masoko, Omari Salisbury |
Na Prince Akbar
BALOZI wa kampuni ya Glenmorangie, Bwana Niel Hendriksz, amewasili
leo hapa Dar es Salaam kwa ziara ya siku mbili ikiwa ni katika ziara yake ya
siku tano katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Dhumuni ya ziara
yake ni kuwazawadia wanywaji wa Glenmorangie pamoja na kuwaelimisha na kujenga
uelewa kuhusu utumiaji wa vinywaji vya Glenmorangie katika ukanda huu wa Afrika
Mashariki.
Glenmorangie inafahamika
kama kinywaji cha wiski pekee ya kutoka Skotland (Single Malt Scotch Whiskey) tamu
na inayopendwa zaidi duniani. Ikiwa imejijengea umaarufu kama mojawapo ya wiski
za awali kabisa, hasa kwa kuweza kuchanganya mbinu za kitamaduni
pamoja na ugunduzi mpya wa kisasa kujitengenezea jina lake maarufu la
‘Unnecessarilly well made’, imekuwa moja ya wiski pendwa zaidi hapa nchini.
Katika ziara yake
hiyo ya siku mbili nchini, Hendriksz atakutana na wapenzi wa wiski katika matukio
mbalimbali maalumu ikiwemo chakula cha mchana katika hoteli ya Dar Es Salaam
Serena ambayo itawapa wapenzi wa Glenmorangie nafasi ya kuonja aina mbalimbali
za wiski kutoka Glenmorangie.
Pia Hendriksz anatarajiwa
kutoa mafunzo maalumu kwa baadhi ya wahudumu kutoka katika bar kubwa ambayo
yatagusa sio tu katika uchanganyaji sahihi wa wiski za Glenmorangie bali pia
historia fupi na aina tofauti za Glenmorangie.
Lengo kuu la mafunzo
hayo ni kuwapa wahudumu ujuzi utakaowawezesha kutoa huduma bora na ya kipekee kwa
wateja wao wakati wakiburudika na Glenmorangie kwenye bar au hotel
wanazozipendelea.
Balozi huyo pia
anatarajiwa kupita katika sehemu mbalimbali zinazouzwa Glenmorangie kujibu
maswali kutoka kwa umma pamoja na kuwapa aina tofauti ya kinywaji hicho wale
ambao hawajawahi kuonja kinywaji hicho.
Lakini kikubwa zadi
kinachosubiriwa katika ziara hii ni tukio litakalofanyika jumanne usiku katika
hoteli ya Hyatt Regency ambapo Hendriksz atafanya sherehe maalumu ya kuonja na
kulinganisha vinywaji vya Glenmorangie.
Huku kukiwa na nafasi
ishirini tu kwa nchi nzima kuhudhuria sherehe hiyo, uhitaji baina ya wapenzi wa
Glenmorangie kuhudhuria umekuwa mkubwa sana. Uonjaji rasmi wa kinywaji cha Glenmorangie
utajumuisha kuonja ladha iliyokomaa vema ya vichanganyishi vya Glenmorangie huku
ukipitia katika ladha tofauti tofauti, harufu pamoja na vionjo mbalimbali
vinayoikamilisha Glenmorangie ikifuatiwa na chakula cha jioni maalumu
kinachoendana sambamba na Glenmorangie.
Zoezi hili limebuniwa
maalumu ili kuwafundisha wanywaji wa Glenmorangie namna ambavyo watafurahia zaidi
kinywaji chao cha Glenmorangie.
Ziara ya Hendriksz itamalizika
jumatano asubuhi hapa nchini ambapo ataelekea Nairobi kwa mwendelezo wa ziara
hiyo hapa Afrika Mashariki.
####
Kwa maelezo zaidi
kuhusu ziara ya balozi wa Glenmorangie tafadhali piga simu no: +255774637777 au
tuma barua pepe kwenda: marketing@qway-international.com
Glenmorangie ni nini?
Glenmorangie ni, kwa urahisi kabisa, aina
ya kinywaji (wiski) yenye ladha nzuri na tamu kuliko yoyote ulimwenguni.
Harufu yake nzuri na ladha ya kipekee
huchangamsha akili na kuifanya uifurahie wakati wa kuinywa.
Ikiwa na mchanganyiko wa kipekee zaidi
ambao unaifanya kuwa kinywaji (wiski) itakayokuachia kumbukumbu ya pekee katika
ladha, mchanganyiko na harufu nzuri.
Kuhusu kampuni ya Glenmorangie
Kampuni ya Glenmorangie ni mojawapo ya
kampuni mashuhuri katika ubunifu na uuzaji wa bidhaa za wiski duniani kote na ni
sehemu ya Moët Hennessy, kitengo cha mvinyo na pombe kali cha Moët Hennessy
Louis Vuitton (LVMH).
Makao yake makuu yako Edinburgh,
Scotland, na Kampuni ya Glenmorangie pia inazalisha Glenmorangie Single Highland
malt whiskey na Ardbeg Single Islay malt. Pia ndio wamiliki wa Scotch Whisky
Malt Society.
Wajibu wa mnywaji
Kampuni ya Glenmorangie
inasimamia unywaji makini na inashauri wanywaji wa Glenmorangie na Ardbeg
whiskeys kunywa kwa kiasi na kwa kuzingatia miongozo iliyopendekezwa ya kiasi
cha pombe kwa siku.