| ||
Joleon Lescott |
Mario Balotelli na wachezaji wenzake kadhaa nyota wa Manchester City usiku wa Jumatatu waliacha vitanda na kwenda kujirusha kwenye shoo la Nicki Minaj.
Rapa huyo wa Marekani, Minaj, ambaye miongoni mwa vibao vyake vikali ni Super Bass na Starships, alivutia nyota wenye majina makubwa katika shoo yake na Balotelli aliikuwa miongoni mwao pamoja na Joe Hart, Gareth Barry, Micah Richards na Joleon Lescott.
Balotelli akiondoka kwenda Uholanzi huku akisiliza muziki |
Kikosi cha City kilichoshinda, 2-1 dhidi ya West Bromwich Jumamosi, kimeondoka kwenda Amsterdam leo kwa ajili ya mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya wenyeji Ajax kesho.
Kikosi cha Roberto Mancini kinamenyana na mabingwa hao wa Uholanzi baada ya kuanza vibaya kampeni yao, wakifungwa na Real Madrid na kut9ka sare nyumbani na Borussia Dortmund.
Micah Richards (kushoto) na James Milner wakiwa Manchester Arena
Balotelli alionekana Uwanja wa ndege na headphones zake za ranfi ya pinki tayari kwa safari ya Uholanzi.
Wakati huo huo, Lescott anataka wakacheze kwa kujituma ili kuepuka aibu kama ya msimu uliopita walipong'olewa katika hatua ya makundi tu.
Joe Hart
Nicki Minaj akipagawishaJijini Manchester juzi katika shoo lililohudhuriwa na nyota wa Man City
SOURCE: http://www.dailymail.co.uk