![]() |
Bahanuzi nyuma ya Kapombe |
Na Princess Asia
MABINGWA wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba SC kesho katika mchezo wao dhidi ya
JKT Oljoro ya Arusha watawakosa wachezaji wao wanne, wakiwemo beki Shomary Kapombe
aliyeumizwa na mshambuliaji Said Bahanuzi wa Yanga Jumatano na Mrisho Ngassa,
ambaye ana Malaria.
Ofisa Habari
wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga amesema leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari,
makao makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Msimbazi kwamba, mbali na nyota hao wawili,
wengine watakaokosekana kwenye mechi ya kesho ni mabeki Amir Maftahi anayetumikia
adhabu ya kadi na Haruna Shamte, ambaye pia ni majeruhi.
Kamwaga alisema
kwamba Kapombe aliumizwa na mshambuliaji wa Yanga, Said Bahanuzi Jumatano
katika mechi baina ya watani hao wa jadi wa soka ya Tanzania, iliyopigwa Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya 1-1.
Kuhusu Ngassa,
Kamwaga alisema kwamba baada ya mechi hiyo ya Jumatano, naye amepata Malaria,
ambayo itamuweka nje ya Uwanja kesho, wakati Haruna aliumia mazoezini, timu
hiyo ilipokuwa kambini Zanzibar ikijiandaa na mechi ya Yanga.
Lakini Kamwaga
alisema pamoja na kuwakosa nyota hao, anaamini wachezaji wengine watakaochukua
nafasi zao watafanya vizuri. Kumbuka Emmanuel Okwi amemaliza adhabu na kesho anaweza
kuiongoza Simba kwenye mechi hiyo.
0 comments:
Post a Comment