Bunjak |
Na Mahmoud
Zubeiry
AZAM FC, washindi
wa Medali tatu za Fedha, Ligi Kuu msimu uliopita, Kombe la Urafiki na Klabu
Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, wameimarisha benchi lao la
ufundi kwa kuleta kocha mpya kutoka Serbia, Slobodan.
Slobodan ametua
Azam kwa kazi moja tu maalum, kuwanoa makipa wa timu hiyo inayofukuzana na
Simba kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Slobodan ni
chaguo la kocha wa sasa wa Azam, kutoka Serbia pia, Boris Bunjak ambaye amerithi
mikoba ya Muingereza Stewart Hall aliyefukuzwa Julai mwaka huu.
Bunjak
mwenye leseni ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), alitua Azam, akitokea FC
Damac ya Saudia Arabia aliyoanza kuifundisha mwaka jana na kabla ya hapo
alifunisha klabu za kibao, zikiwemo FK Sloga Kraljevo, FK Javor Ivanjica,
Crvena Zvezda Gnjilane, FK Radnicki Nis, FC Uralan Elista, FK Mladi Radnik, FK
Crvena Zvezda Beograd, Al-Shaab, FK Hajduk Kula na Al-Nasr.
Awali,
Bunjak aliyezaliwa Novemba 17, mwaka 1954 ( miaka 57), alicheza soka katika
klabu za FK Sloga (Kraljevo), FK Vozdovac (Beograd), FK Radnicki (Kragujevac),
FK Olimpia (Ljubljana), FK Sumadija (Arandjelovac), FK Sloga (Kraljevo), FK
Borac (Cacak) na FK Sloga (Kraljevo).
Mserbia huyo
anakuwa kocha wa tano Azam, ndani ya miaka minne tangu ianze kucheza Ligi Kuu,
2008 baada ya Stewart, Mbrazil Neider dos Santos, Sylvester Marsh na Itamar
Amorin, Mbrazil mwingine.
Lakini ni
Stewart angalau anaacha kumbukumbu ya taji na Medali za Fedha Azam, baada ya
kuiwezesha kutwaa Kombe la Mapinduzi Januari mwaka huu, kushika nafasi ya pili
katika Ligi Kuu Mei mwaka huu, kabla ya kushika nafasi ya pili Kombe la Urafiki
na Kagame Julai mkwaka huu.
Bunjak alitambulishwa
Azam Agosti 7, mwaka huu na akaanza kufundisha timu siku iliyofuata na hadi
sasa amekwishaiongoza timu katika mechi 11 na kushinda saba, sare moja na
kufungwa mbili, zote dhidi ya Simba SC moja kwenye Nusu Fainali ya Kombe la
BancABC Sup8R 2-1 na nyingine ya Ngao ya Jamii 3-2.
REKODI YA BORIS BUNJAK AZAM
Azam 2-1
Polisi Moro (BancABC)
Azam 1-2
Simba B (BancABC)
Azam 8-0
Transit Camp (Kirafiki)
Azam 1-0
Prisons (Kirafiki)
Azam 2-0
Coastal Union (Kirafiki)
Azam 2-3
Simba SC (Ngao ya Jamii)
Azam 1-0
Kagera Sugar (Ligi Kuu)
Azam 2-2
Toto African (Ligi Kuu)
Azam 3-0 JKT
Ruvu (Ligi Kuu)
Azam 1-0
Mtibwa Sugar (Ligi Kuu)
Azam 1-0
African Lyon (Ligi Kuu)