Azam FC |
Na Prince Akbar
KLABU ya Azam imeomba mechi zake za
nyumbani dhidi ya Yanga na Simba zichezwe kwenye Uwanja wake wa Chamazi,
maarufu kama Azam Complex ulioko Chamazi badala ya Uwanja wa Taifa.
Kuhusu maombi hayo, Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) limesema yatawasilishwa kwenye kikao cha Kamati ya Ligi ya
TFF kinachotarajiwa kufanyika leo mjini Dar es Salaam.
TFF iliamua mechi zote za Simba na
Yanga dhidi ya timu za Dar es Salaam na Pwani, zichezwe kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam kwa sababu ya idadi kubwa ya mashabiki wanaotarajiwa kuingia
uwanjani, wakati viwanja vya Chamazi na Mabatini, Mlandizi unaotumiwa na Ruvu
Shooting ni vidogo.
Awali, TFF ilipanga Ruvu Shooting
na Yanga zicheze kwenye Uwanja wa Chamazi pia Oktoba 20, mwaka huu, lakini
klabu hiyo inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kitengo cha Jeshi
la Kujenga Taifa (JKT), imeomba mechi hiyo ichezwe Uwanja wa Taifa.
Ingawa Ruvu Shooting haijasema
sababu za kuomba mechi hiyo ichezwe Taifa badala ya Chamazi, lakini dhahiri
wanataka kunufaika na mapato kutokana na ukubwa wa Uwanja wa Taifa.