Arsenal imekuwa ikidhaminiwa na Nike tangu 1994
Nembo tatu; Arsenal inajiandaa kuingia mkataba na Adidas
KLABU ya Arsenal inaelekea kumaliza ushirikiano wake wa miaka 18 na kampuni ya Nike na kusaini mkataba mpya wa pauni Milioni 25 na wapinzani wa kampuni hiyo ya vifaa vya michezo, Adidas.
The Gunners imekuwa ikidhaminiwa na kampuni hiyo ya Marekani, Nike tangu mwaka 1994, lakini Adidas, ambao ni wadhamini wa wapinzani wao, Chelsea, wanajiandaa kuichukua klabu hiyo.
Kwa mujibu wa The Daily Telegraph, nembo hiyo ya Ujerumani itafufua uhusiano wake na Arsenal wakati klabu hiyo ya London itakapomaliza mkataba na Nike mwaka 2014.
The Daily Telegraph limeripoti kwamba Fulham, inayodhaminiwa na Kappa, itaungana na Adidas pia, katika mpango wa kampuni hiyo ambao unachukuliwa kama wa kuliteka Jiji la London kisoka.
Mbali na Manchester United na Barcelona, Arsenal ni klabu kubwa inayouza jezi za Nike kwa mashabiki wasiopungua 800,000 kila mwaka.
Mkataba wa Arsenal na Adidas utawafanya wapokee mara mbili ya fedha walizokuwa wakipewa na Nike, pauni Milioni 13 kwa msimu.
Wanaouza jezi za klabu za Ligi Kuu England
Arsenal - Nike (Marekani)
Aston Villa - Macron (Italia)
Chelsea - Adidas (Ujerumani)
Everton - Nike (American)
Fulham - Kappa (Italia)
Liverpool - Warrior (Marekani)
Man City - Umbro (Uingereza)
Man United - Nike (Marekani)
Newcastle - Puma (Ujerumani)
Norwich - Errea (Italia)
QPR - Lotto (Italia)
Reading - Puma (Italia)
Southampton - Umbro (Uingereza)
Stoke - Adidas (Ujerumani)
Sunderland - Adidas (Ujerumani)
Swansea - Adidas (Ujerumani)
Tottenham - Chini ya Armour
West Brom - Adidas (Ujerumani)
West Ham - Macron (Italia)
Wigan - Mi FIt (Uingereza)