ARSENAL WAMUITA FARAGHA WALCOTT BAADA YA KUWAPIGIA HAT TRICK YA MAANA
Arsenal inajiandaa kukutana na mshambuliaji wake, Theo Walcott, mwenye umri wa miaka 23, wiki ijayo kujaribu kumzuia mchezaji huyo wa kimataifa wa England kuondoka mkataba wake utakapomalizika msimu ujao.
Manchester United inafuatilia uchezaji wa kiungo wa Bayer Leverkusen, Lars Bender. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 aliibukia katika timu hiyo ya Ujerumani msimu uliopita na kucheza soka ya nguvu Leverkusen.
QPR inataka kumsajili beki wa Real Madrid, Ricardo Carvalho, ifikapo Januari. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 34 anayecheza beki ya kati tayari amekwishaambiwa hataongezewa mkataba akimaliza wa sasa mwishoni mwa msimu na anaweza kuamua kurejea Ligi Kuu England.
BERG KOCHA MPYA ROVERS
Beki wa zamani wa Blackburn, Henning Berg anatarajiwa kutajwa kama kocha mpya wa Rovers leo, akirithi mikoba ya Steve Kean, ambaye alijiuzulu Septemba.
Jamaica ina matumaini ya kumshawishi mshambuliaji chipukizi wa Liverpool, Raheem Sterling, mwenye umri wa miaka 17, awachezee wao badala ya England, baada ya kinda huyo kufanya mavitu adimu msimu huu Anfield.